LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 6, 2021

TANZANIA KUISAIDIA BURUNDI KUJIUNGA SADC

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi ameiahidi nchi ya Burundi kuwa Tanzania itashirikiana nayo katika harakati zake za kuomba kujiunga na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Kabudi ametoa ahadi hiyo leo mkoani Kigoma kwenye mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Burundi.

Amesema Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wa kindugu baina ya nchi hizo mbili kama njia mojawapo ya kuwaenzi waasisi wake.

“Njia pekee ya kuwaenzi waasisi wa mataifa haya mawili ni kuimarisha uhusiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, kijamii na masuala ya usalama” Kabud
i

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages