LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 19, 2021

RAIS SAMIA ATANGAZA RATIBA YA MAZISHI YA HAYATI DK. MAGUFULI ATAKAYEZIKWA CHATO, GEITA, MACHI 25, 2021

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia Taifa, baada ya kuapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Ikulu Dar es Salaam
Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🇹🇿Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ametangaza ratiba nzima ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dk. John Magufuli aliyefariki Dunia juzi, Jijini Dar es Salaam.

Rais Samia ametangaza ratiba hiyo, wakati akilihutubia Taifa baada ya kuapishwa kuwa Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo.

Ratiba hiyo ni kama ifuatavyo:,

😭Kesho Jumamosi, Machi 20, 202 mwili wa Hayati Dk. John Magufuli utatolewa Hospitali ya Jeshi Lugalo Jijini Dar es Salaam na kupelekwa katika Kanisa la Matakatifu Peter kwa ajili ya ibada na kisha kupelekwa Uwanja wa Uhuru kuendelea na taratibu za kuuaga mwili.

😭Jumapili, Machi 21, 2021, Wananchi wa Dar Es Salaam wataaga mwili wa Dk. Magufuli katika Uwanja wa Uhuru na baadaye utasafirishwa kwenda Makao Makuu ya nchi, Jijini Dodoma.

😭Jumatatu Machi 22, 2021 Mwili wa aliyekuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Hayati Dk. Magufuli, utaagwa Jijini Dodoma na kisha kusafarishwa kwenda jijini Mwanza.

😭Jumanne Machi 23, 2021, mwili utaagwa jijini Mwanza na baadaye siku hiyo hiyo kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Chato, mkoani Geita.

😭Jumatano Machi 24, 2021 wanafamilia wa Hayati Dk. Magufuli na Wananchi wa Chato na mikoa ya jirani, watauaga mwili.

😭Alhamisi Machi 25, 2021 shughuli za mazishi zitafanyika Chato mkoani Geita.

😭Pumzika kwa amani Hayati Dk. John Magufuli. Nenda mwamba!💪

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages