LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 18, 2021

MWONGOZO WA KATIBA YA TANZANIA KUHUSU KUPATA RAIS MWINGINE, RAIS ANAPOFARIKI DUNIA

Hayati Dk. John Magufuli

Dar es Salaam, Tanzania

Baada ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kutangaza jana kifo cha Rais Dk. John Magufuli, akisema Magufuli amefariki dunia saa 12 jioni kwa maradhi ya moyo baada ya kulazwa katika hospitali hiyo tangu Machi 6, mwaka huu, Watanzania wamepokea taarifa hizo kwa mshutuko mkubwa.


Watanzania wamepokea taarifa hizo kwa mstuko na simanzi kubwa kutokana na kwamba Dk. John Magufuli hakika alikuwa kipenzi cha Watanzania, hasa wanyonge. 


Kwa ufupi alikuwa Rais ambaye alionyesha matumaini yasiyopingika kwa kuwa utendaji wake ulinyeshea sekta mbalimbali na kuzaa mwanga mkubwa wa matumaini ya neema tele kwa Tanzania ya baadaye.


Lakini, pamoja na kutingwa na majonzi makubwa baada ya taarifa hizo, wapo Watanzania wengi ambao wamekuwa wakijiuliza au kuuliza kwamba, je, kufuatia kifo cha kipenzi chao Rais, utaratibu ukaofuata kumpata Rais mwingine ni upi?


Kwa bahati nzuri Tanzania inao utaratibu ambao upo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo kwa mujibu wa katika hiyo, baada ya kufariki Dunia, Makamu wa Rais ndiye ambaye anashika nafasi ya Kuwa Rais baada ya kuapishwa.


Kwa hiyo kufuatia Rais Dk. John Pombe Magufuli kufariki dunia, hakuna uchaguzi mwingine unaofanyika badala yake, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ataapishwa kuwa Rais kwa kipindi kilichosalia katika muhula wa miaka mitano.


Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 37 (5), baada ya Samia kuapishwa atashauriana na chama anachotoka ambacho ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kisha atamteua mtu atakayekuwa Makamu wa Rais. 


Ibara ya 37 (5) ya katiba imeandikwa kuwa endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kuktekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia 50 ya Wabunge wote.


Kwa mujibu wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages