Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Isdor Mpango ataapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa iiyotolewa na Ikulu jijini Dodoma, imsema, Mpango ataapishwa katika Hafla itakayofanyika Ikulu, Chamwino jijini Dodoma kuanzia saa 9:00 alasiri na itaonyeshwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii
Dk. Mpango ataapishwa kushika wadhifa huo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuwasilisha mapendekezo ya jina la Dk. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais katika Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi na baadaye jina hilo kuwasilishwa Bungeni na kupitishwa kwa asilimia 100 ya kura
Bungeni
Akitangaza matokeo baada ya wbunge kupiga kura leo za kumthibitisha Dk. Mpango kuwa Makamu wa Rais, Spika wa Bunge Job Ndugai alisema kuwa jina la Dk. Mpango limethibitishwa kwa asilimia 100 kwani wabunge waliopiga kura ni 363 na sasa anasubiri kuapishwa na Jaji Mkuu.
Kabla ya kutangaza matokeo hayo, Spika Ndugai alimpa nafasi Dk.Mpango ya kuzungumza kwa mara mwisho ndani ya Bunge hilo kwani baada ya hapo hataruhusiwa kuzungumza chochote kwa mujibu wa Katiba.
Kabla ya kumkaribisha Dk. Mpango, Spika Nduga aliwaambia wabunge kwa mujibu wa Katiba jina lake likashapitishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hataweza kuzungumza bungeni, hivyo ni vema akazungumza kabla ya jina kuthibitishwa na Bunge.
"Nimehangaika sana kupata jibu la nini tufanye, nimeangalia katiba yetu inaeleza wazi kabisa, hivyo tukisubiri athibitishwe na Bunge kisha aseme haitawezekana, hivyo azungumze kabla jina halijathibitishwa.Kuna watu huko nje huko wataanza kusema Spika hakufuata Katiba.Dk.Mpango karibu uzungumze na wabunge kwa mara mwisho humu ndani,"alisema Spika Ndugai.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇