KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Zainab Chaula akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Wadau kujadili mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ya TEHAMA jijini Dodoma Machi 16, 2021. Kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria wa wizara hiyo, Lugano Rwetaila na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara, Godleader Shoo..
Baadhi ya wadau wakisikiliza kwa makini wakati Katibu Mkuu, Dk. Chaula akizungumza.
Katibu Mkuu Dk. Chaula akiwa na wadau mbalimbali katika picha ya pamoja
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Zainab Chaula amefungua kikao kazi cha Wadau kujadili mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ya TEHAMA jijini Dodoma Machi 16, 2021.
Amesema kuwa sheria hiyo ikitungwa itasaidia kuboresha mfumo wa mawasiliano katika sekta mbalimbali nchini, hivyo kuitoa nchi kutoka uchumi wa kati na kuipeleka uchumi wa juu.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau kutoka sekta binafsi na maofisa wa Serikali.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Dk. Chaula akizungumzia umuhimu huo wa uboreshaji wa Tehama na Mkono wa Taifa...
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇