Na Crispin Gerald
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imekamilisha kazi ya kuunganisha bomba kubwa la inchi 10 maeneo ya daraja la kinyerezi litakalopokea maji kutoka kwenye mradi mkubwa wa maji wa Pugu-Gongo la mboto kwa ajili ya kuhudumia wakazi wa maeneo ya Kinyerezi, Mongo la ndege, Kifuru na Vindini.
Zoezi la kuunganisha bomba ni sehemu ya kazi inayoendelea ya kujenga mtandao wa kupokea maji kutoka kwenye tanki la Maji Pugu na utakaohudumia wakazi takribani 1,000 wa maeneo hayo.
Akizungumzia zoezi hilo Meneja wa Usambazaji Mhandisi Tyson Mkindi amesema kazi iliyofanyika ni kubadilisha mtandao wa maji uliokuwepo kwa kuweka bomba lipya la inchi 10 litakaloweza kupokea na kusambaza maji.
“Kazi imekamilika na baada ya kukamilisha kujenga mtandao tutaruhusu maji yaweze kufika kwa wananchi,” alisema.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇