LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 9, 2021

ATLAS SCHOOLS MADALE WAFANYA UCHAGUZI WAO WA RAIS 2021/2022, WAGOMBEA WACHUANA VIKALI KUOMBA KURA, ABUBAKAR HAJJ ATWAA KITI

Atlas Madale, Dar es Salaam

Wanafunzi wa Atlas Schools Kampasi ya Madale jijini Dar es Salaam, hivi karibuni wamefanya Uchaguzi wa Rais 2021/2022 na Abubakar Hajj kuchanguliwa kuwa Rais wa Wanafunzi hao, baada ya kuongoza kwa kupata kura 687 sawa na asilimia 54.9 dhidi ya mgombea mwenzake.


Katika uchaguzi huo ambao ulivutia kwa wagombea hao wawili kuonyesha weledi mkubwa hasa wakati wa kujieleza wakiomba kura kwa wanafunzi wenzao, Abubakar alichuana vikali na mgombea mwenzake wa nafasi hiyo ya Urais, Fanny Foster aliyepata kura 544 sawa na asilimia 43.5.


Jumla ya kura zilizopigwa  zilikuwa 1251, zikiharibika 20 na kura halali kubakia 1231 ambapo kufuatia uchaguzi huo Abubakar alitangazwa kuwa  Rais wa Wanafunzi wa Atlas Kampasi ya Madale kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 huku Angel Boniventura akitangazwa kuwa Makamu wa Rais Atlas Madale 2021/2022. 

Habari katika Picha👇

Aliyekuwa Mgombea wa Urais Atlas Madale 2021/2022 Abubakar Hajj akiomba kura kwa wajumbe, wakati wa Uchaguzi huo.

Mgombea Urais Atlas Madale 2021/2022 Fanny Foster akiomba kura kwa wajumbe katika Uchaguzi huo.
Mpigakura Kauthar Haji Abuu wa Std Six Red akimuuliza swali Abubakar Hajj
Mpigakura akimuuliza swali  Abubakar
Mpigakura Rahma Mohammed akimuuliza swali Mgombea Fanny Foster wakati wa uchaguzi huo.

Wapigakura ambao ni wanafunzi wa Atlas Madale wakiwa kwenye Uchaguzi huo.


Upigaji kura ukifanyika baada ya Wagombea kuomba Kura

Chini ni 'Video Clip'  Abubakar na mwenzake Fanny wakionyesha umahiri wao wakati wakichuana kuomba kura. Tafadhali, Bofya Hapo👇




No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages