LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 14, 2021

ALIYEZUSHA KUWA RAIS MAGUFULI NI MGONJWA AKAMATWA

 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Ramadhani Kingai amesema Polisi wanamshikilia Charles Majura (35) ambaye ni Fundi Simu, kwa kosa la kimtandao kwa kusambaza taarifa za uzushi kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni Mgonjwa.

Kamanda Kingai amesema kumekuwa na tabia ya baadhi wa Watu pindi wanapotumiwa taarifa za uzushi nao wanasambaza bila kujua kuwa ni kosa kisheria na kusema wanaendelea kuwafuatilia wote wenye tabia hiyo na wakikamatwa watafikishwa Mahakamani.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages