LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 16, 2021

WAZIRI WA ZAMANI NA MWENYEKITI WA KWANZA WA UVCCM, DK. MOHAMMED SEIF KHATIB AZIKWA LEO MJINI ZANZIBAR😭😭

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiweka udongo katika kaburi wakati wa maziko ya Waziri wa zamani na Mwenyekiti wa kwanza wa Umoja wa Vijana wa CCM, Mohammed Seif Khatib,yaliofanyika Kijijini kwao Umbuji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, leo. Dk. Khatib alifariki jana.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akishiriki kuitikia dua katika Hitma yakumuombea Marehemu Mohammed Seif Khatib katika Msikiti wa Masjid Noor Muhammad S.A.W. Mombasa kwa Mchina mwanzo mjini Zanzibar  kabla ya kwenda mazikoni, leo. Wengine ni  Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla na Rais Mstaaf wa Zanzibar.Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Balozi Seif Ali Iddi Makamu wa Pili wa Rais Mstaaf na Mtoto wa Marehemu, Seif Mohammed Seif.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Kiislam katika Sala ya Jeneza ya kumuombea Marehemu Mohammed Seif Khatib ikiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi, iliofanyika katika Masjid Noor Muhammad SAW kwa mchina mwazo. Kulia kwa Rais ni Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla na Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhajj Dk. Mohamed Ali Shein na kushoto kwa Rais ni Katibu Ofisi ya Mufti Mkuu Sheikh Abdalla Talib na Alhajj Balozi Seif Ali Iddi Makamu wa Pili wa Rais Mstaaf, wakishiriki katika Sala hiyo.
WAUMINI wa Kiislam wakiitikia dua baada ya kumaliza kwa Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Mohammeed Seif Khatib iliofanyika katika Masjid Noor Muhammad S.A.W kwa Mchina mwanzo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa marehemu Mohammed Seif Khatib ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman, iliofanyika katika Masjid Noor Muhammad S.A.W kwa mchina mwazo. na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein wakiitikia dua
VIJANA wa UVCCM wakiwa wamebeka jeneza likiwa na mwili wa marehemu Mohammed Seif Khatib, wakielekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya maziko yake yaliofanyika Kijijini kwao Umbuji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
WANANCHI wakishiriki katika maziko ya marehemu Mohammed Seif Khatib yaliofanyika Kijijini kwao Umbuji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.leo 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ya kumuombea Marehemu Mohammed Seif Khatib na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhajj Dk. Ali Mohamed Shein, wakiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalib Ali Mfaume, baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliofanyika Kijijini kwao Umbuji Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.(Maelezo na Picha zote na Ikulu, Zanzibar).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages