Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika, Younouss Djibrine ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma leo Februari 16,2021 ambaye wamekutana kuzungumzia uboreshaji wa huduma za Posta hapa nchini.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika, Younouss Djibrine (kulia) ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma leo Februari 16, 2021 ambaye wamekutana kuzungumzia uboreshaji wa huduma za Posta hapa nchini. kushoto Katibu Mkuu wizara hiyo Dkt Zainabu Chaula.
Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile leo amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mashirika ya Posta Afrika (PAPU), Younouss Djibrine na kufanya naye mazungumzo kwenye ofisi ya wizara hiyo katika Mji wa Kiserikali wa Mtumba, jijini Dodoma.
Pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu amesema kuwa nia ya kukutana naye ni kumpongeza Waziri Ndugulile kwa kuteuliwa na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo mpya pamoja na kumueleza hatua iliyofikiwa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika jijini Arusha.Jengo hilo linajengwa kwa ushirikiano wa PAPU na Serikali ya Tanzania.
Aidha, Waziri Ndugulile amesema kuwa pamoja na mambo mengine wamekubaliana na Katibu Mkuu huyo wa PAPU namna bora ya kuziendesha huduma za posta na namna ya kuboresha huduma za posta katika kuziendesha kidigitali na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Sayansi na teknolojia.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video yaliyojiri kwenye kikao hicho wakati Waziri Ndugulile na Katibu mkuu wa PAPU, Djibrine wakizungumza na vyombo vya habari leo Februari 16...
IMEANDALIWA NA: RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇