Serikali imepiga marufuku shughuli zote zisizo za kiuhifadhi zinazofanywa na binadamu katika maeneo yaliyohifadhiwa nchini kwakua maeneo hayo ni sehemu ya mapato na vivutio nchini.
Marufuku hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja wakati akijibu swali la Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei bungeni mapema leo
Amesema serikali imeweka maeneo ambayo ni sahihi kwa matumizi ya kibinadamu na si kufanya shughuli zisizo za kiuhifadhi ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa nchini
“Sisi kama serikali tunapokua tunahifadhi haya maeneo, tunatunza ili yawe kivutio na kwa ajili ya kutuletea mapato, kwahiyo tunapotukua tunatunza hairuhusiwi kufanya kitu chochote ndani ya eneo la hifadhi, hataka kama ni kuokota kuni hairuhusiwi, lakini kuna maeneo mengine ambayo huwa tunawatengea wananchi kwa ajili ya kuendelea na shughuli zingine kama ufugaji, Uvuvi pamoja na Kilimo, lakini maeneo yanayotunzwa kama hifadhi hairuhusiwi kufanya Chochote” Amesema Mhe. Mary Masanja
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇