LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 3, 2021

RAIS MAGUFULI ATAKE ASITAKE ATAONGEZEWA KIPINDI CHA KUONGOZA-MBUNGE SANGA

Mbunge wa Makambako, Deo Sanga akizungumza Bungeni Dodoma leo na kutaka Rais Magufuli aongezewe kipindi cha kuongoza nchi kutokana na kazi nzuri aliyoifanya  kwa miaka mitano ya uongozi wake.
 

Na Richard Mwaikenda, Dodoma

MBUNGE wa Jimbo la Makambako, Deo Sanga amesema kuwa Rais John Magufuli atake asitake ataongezewa kipindi kingine cha kuiongoza nchi.


Sanga ameyasema hayo bungeni Dodoma leo alipokuwa akichangia hotuba ya Rais Jonh Magufuli aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 12 Novemba 2020.


Amesema kuwa kuongezewa muda wa kuongoza kwa Rais Magufuli si dhambi, kwani anatakiwa aendelee kuingoza nchi.


Baada ya Mbunge Sanga kumaliza kuzungumza, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson alisema kuwa Rais Magufuli alishatoa msimamo wake kuhusu jambo hilo, ila wabunge ni hawazuiwi kuzungumzia.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages