LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 16, 2021

SERIKALI KAMWE HAITAKUWA KIKWAZO: WAZIRI UMMY

 


Serikali imesema kamwe haitakuwa kikwazo kwa wawekezaji katika kutoa vibali vya Tathmini ya Athari kwa mazingira katika kuwezesha uwekezaji na maendeleo ya viwanda. Kauli hii imetolewa hii leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano ana Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kukagua shughuli za utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira.

Amesema azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira Rafiki kwa wawekezaji na kutoa miongozi katika hifadhi ya mazingira na kuliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutoa ushauri wa kitaalamu kuwezesha wawekezaji kuzingatia Sheria.

“NEMC simamieni Sheria ya Mazingira, Viwanda visiwe sehemu ya uchafuzi wa Mazingira ili Maendeleo ya Viwanda yaendane na Hifadhi ya Mazingira pia NEMC msifanye kazi ya upolisi kwa kufunga Viwanda na kutoza faini kubwa, kaeni na wenye Viwanda waelekezeni kuzingatia Sheria Waziri Ummy alisisitiza.

Akimkaribisha katika Mkoa wa Pwani Mkuu wa Mkoa Mhandisi  Evarist Ndikilo amesema Mkoa wake unakabiliwa na changamoto kubwa ya ukataji miti kutokana na matumizi ya kuni na mkaa na kutoa rai kwa Wizara kuangalia uwezekano wa kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ikiwemo gesi. 

Pia ameshauri kuwekwa kwa utaratibu kwa wachimbaji wa mchanga kuhakikisha kunakuwa na urejerezaji wa maeneo ya machimbo kwa kupanda miti ili kuepuka uharibifu wa Mazingira . Waziri Ummy amesisitiza kuwa Agenda ya Mazingira ni suala mtambuka na kutoa rai kwa uongozi wa Mkoa wa Pwani kutumia Sheria ndogo za Halmashauri kusimamia.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages