Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Leonald Subi akitoa tahadhari ya kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa corona na mengineyo kwa kuzingatia ushauri wa watalaamu. |
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza kwa makini RC Dk. Mahenge akizungumza na kuwapa maagizo.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge amesikitishwa na idadi kubwa ya vifo vya akina mama na watoto Kanda ya Kati, hivyo kuwataka watalaamu wa afya wanaohudhuria mkutano wa kujadili hali ya afya na Uzazi na Mtoto kupanga mikakati ya kupunguza au kuzuia vifo hivyo.
RC Dk. Mahenge alitoa akigizo hilo wakati wa mkutano huo ambao pia uliwashirikisha wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya za mikoa ya kanda ya kati ulioanza leo jijini Dodoma. Ametaja Takwimu za ongozeko hilo tangu mwaka juzi hadi sasa na kubainisha piansababu zinzochangia ongezeko la vifo hivyo kuwa ni; kumwaga damu nyingi wakati wa kujifungua,kifafa cha mimba, kushuka kwa mji wa uzazi na maambukizo mengine ambavyo hata hivyo vinaweza kuzuilika. "Nataka kikao hiki kipange mikakati inayofahamika ya kupunguza au kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi, mfanye kila linalowekana la kumsaidia mama mzazi kuepukana na vifo hivyo,"amesema Dk. Mahenge.Ndugu nakuomba uendelee kumsikiliza RC Mahenge kupitia clip hii ya video ujue zaidi maagizo aliyoyatoa kwa watalaam hao wa afya....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇