LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 22, 2021

MAKAMU WA RAIS SAMIA KUFUNGUA KONGAMANO LA CHAMA CHA WATALAAMU WA MAENDELEO YA JAMII DODOMA

 

Rais wa Chama cha Watalaamu wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (CODEPATA), Wambura Sunday akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, jijini Dodoma leo kuhusu maandalizi ya mkutano mkuu na kongamano lao litakaloanza kesho Jumanne jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa CODEPATA, Pascal Mahinyila akifafanua jamo wakati wa mkutano huo.


Na Richard Mwaikenda, Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mama Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu pamoja na Kongamano la Chama cha Watalaamu wa Maendeleo ya Jamii ,(CODEPATA) jijini Dodoma Jumatano. Pamoja na mambo mengine katika kongamano hilo watampongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake mzuri wa kuliletea Taifa Maendeleo lakini pia katika uchaguzi mkuu watahakikisha wanawachagua viongozi wa chama hicho wenye kasi ya kufanya kazi kama Rais huyo wa awamu ya Tano. Rais wa Chama hicho Wambura Sunday, akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma leo, amesema kuwa katika kongamano hilo watajadili mada mbalimbali zikiwemo; Elimu ya Lishe ya Jamii, Bima ya Afya iliyoboreshwa,• Mila na desturi zenye kuleta madhara kama vile ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni zinavyokinza na maendeleo . Ndugu msomaji nakuomba uendelee kusoma taarifa yao iliyotolewa kwenye mkutano huo na vyombo vya habari pamoja na kuwasikiliza viongozi wa chama hicho wakizungumzia yatakayojiri kwenye mkutano na kongamano hilo kupitia clip hii ya video.....


CHAMA CHA WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII TANZANIA

DONDOO ZA RAIS WA CHAMA KUFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI

1.0.       UTANGULIZI

Chama cha Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (CODEPATA)  kwa kushirikiana na Wizara tangu mwaka 2017 kimekuwa kikifanya Mkutano Mkuu wa Watalaamu wa Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi katika kutekeleza majukumu ya Sekta ya Maendeleo ya Jamii. Hadi sasa, jumla ya mikutano 3 imekwishafanyika na kuhudhuriwa na wataalam wa kada ya Maendeleo ya Jamii kutoka Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Taasisi za Wizara na Wizara za kisekta na Asasi za Kiraia.

CODEPATA katika kufanikisha Kongamano na Mkutano wa 4 wa wataalam wa maendeleo ya jamii, inaendelea kushirikiana na Wizara pamoja na wadau mbalimbali katika Maandalizi ya Mkutano na Kongamano hilo.

2.0   UMUHIMU WA KONGAMANO NA MKUTANO MKUU WA WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII

Umuhimu wa Kongamano na Mkutano huu ni kukutanisha Wanachama wa Chama cha Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii ili kupeana mbinu na mikakati itakayowezesha kutekeleza majukumu yetu kwa ufasaha zaidi. Pia, kubadilishana uzoefu na mbinu mpya zinazoibuka katika kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika jamii.

3.0   LENGO KUU LA MKUTANO

Lengo kuu la Kongamano na Mkutano ni kuboresha utendaji kazi wa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kwa Maendeleo endelevu.

3.1      MALENGO MAHUSUSI

·        Kuwakutanisha wanachama wa CODEPATA kutoka sehemu mbalimbali za nchi

·        Kubadilishana uzoefu na mbinu mpya za kiutendaji, kujengeana uwezo, na kuimarisha ushirikiano wa wataalamu wa Maendeleo ya Jamii na matumizi ya teknolojia katika uhamasishaji wa kazi za maendeleo ya jamii na wadau wengine.

·        Kupata uzoefu wa shughuli za Maendeleo ya jamii kwa vitendo; Kujadili matokeo ya tafiti kutoka Vyuo vinavyotoa taaluma ya Maendeleo ya Jamii zinazohusiana na sayansi ya jamii.

·        Kuwasilishwa kwa mada mbalimbali zenye lengo la kubadilishana uzoefu baina ya Wanachama na Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii

·        Kufanya Mkutano Mkuu wa nne wa Mwaka wa Chama cha wataalamu wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (CODEPATA)

·        Kufanya Uchaguzi Mkuu wa Chama (CODEPATA) wa Mwaka 2021

 

5.0 KAULI MBIU

Kauli mbiu ya Kongamano na Mkutano ni;

“Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii ni Nguzo ya kujenga Jamii yenye kujitegemea katika kuimarisha Uchumi wa Kati”

 

6.0. SHUGHULI ZITAKAZOFANYIKA

·        Kumpongeza Mh. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuhamishia kwa vitendo Makao Makuu ya Nchi jijini Dodoma.

·        Maonesho ya kazi za  vikundi vya Wajasiriamali, watu binafsi, Asasi za kiraia na Taasisi

·        Uwasilishaji wa mada mbalimbali na majadiliano ambapo mada sita (6) zitawasilishwa na kujadiliwa wakati wa kongamano. Kati ya mada sita (6), mada tatu (3) zitawasilishwa katika majadiliano ya vikundi (parallel sessions).

·        Uzinduzi wa Tovuti ya Chama

·        Mkutano Mkuu wa Chama cha Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA).

·        Uchaguzi Mkuu wa Chama Kuchagua Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu wa Chama, Mweka Hazina na Waratibu wa Kanda 7 za Chama

7.0. WASHIRIKI

 Mkutano unatarajiwa kuwa na washiriki wapatao 400 ambao ni;

·        Wanachama wa CODEPATA kutoka sekta za umma na binafsi.

·        Viongozi na Watumishi wa Wizara

·        Maafisa kutoka Wizara za kisekta na Taasisi za Serikali.

·        Wanachama Kutoka Vyuo Vikuu na vya Kati vinavyotoa mafunzo ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii

·        Wanachama kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’S)

·        Taasisi za Dini

·        Wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi

·        Maafisa Maendeleo ya Jamii mashuhuri

·        Waandishi wa habari

 

8.0 WAGENI RASMI

·        Mgeni Rasmi wa ufunguzi wa kongamano na mkutano amependekezwa awe; Mh. Bi. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

·        Mgeni Rasmi atakayefunga mkutano atakuwa ni; Mhe. Dr. Dorothy Gwajima (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto.

 

9.0   MADA ZA KONGAMANO

9.1   Mada Kuu

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) atawasilisha Mada kuu kuhusu Uongozi wa Kimkakati katika kutekeleza na kusimamia Shughuli za Maendeleo ya Jamii. Aidha, mada hii itaelezea pia kuhusu kaulimbiu ya Mkutano.

9.2     Mada zitakazowasilishwa

·        Uongozi wa Kimkakati katika kutekeleza na kusimamia shughuli za Maendeleo ya Jamii – Wote

·        Mwendelezo wa mada ya Mabadiliko ya fikra na mtazamo katika utekelezaji wa majukumu ya Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii – Wote

·        Matumizi ya Nadharia za kisaikolojia katika kuwezesha Maendeleo ya Jamii - Wote

·        Elimu ya lishe ya Jamii–Wote

·        Bima ya Afya iliyoboreshwa - Wote

·        Mila na desturi zenye kuleta madhara kama vile ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni zinavyokinza na  maendeleo – Wote

·        Maadili na Viwango (Ethics and Standards) vya Wataalam/Taaluma ya  Maendeleo ya Jamii – Wote

·        Tathimini ya utekelezaji wa ugatuaji wa madaraka na ufanisi wa utendaji kazi wa shughuli za Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii– Wote

·        Nafasi ya Wataalamu wa Maendelo ya Jamii katika kuleta mabadiliko chanya katika Jamii – Wote

10. MAHALI NA TAREHE

Kongamano na Mkutano utafanyika tarehe 23-26 Februari 2021 Jiji la Dodoma kwenye Hoteli ya Morena.

11.0 UENDESHAJI WA MKUTANO

Uendeshaji utagawanyika katika sehemu kuu mbili; sehemu ya kwanza itakuwa ni kongamano na sehemu ya pili ni mkutano mkuu.

·        KONGAMANO

·        MKUTANO

AGENDA ZA MKUTANO WA CHAMA (CODEPATA)

             i.        Kufungua Mkutano wa 4 wa Chama

           ii.        Kusoma Muhtasari wa Mkutano wa 3 wa Chama

          iii.        Kusoma Yatokanayo na Mkutano Mkuu wa 3 wa Chama

          iv.        Taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za chama kwa kipindi cha mwaka 2020

           v.        Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Chama kwa Mwaka 2021

          vi.        Agenda zingine kwa Idhini ya Mwenyekiti

        vii.        Kupanga tarehe na mahali pa Kongamano na Mkutano Ujao

      viii.        Uchaguzi Mkuu wa Viongozi Wakuu wa Chama

          ix.        Kufunga Mkutano

 

12. KUWAKARIBISHA WASHIRIKI

Wakaribishe sana washiriki wote wa Kongamano na Mkutano ili waweze kusafiri na kushiriki Kongamano.

IMEANDALIWA NA: RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages