Sabuni iliyotengenezwa kwa mchele
Mkurugenzi wa Zaidat inayoundwa na wajasiriamali 6, Tatu Seleman akizungumza na vyombo vya habari kuhusu bidhaa mbalimbali wanazotengeneza.
Wajumbe wa Bodi na watendaji wa Mkurabita wakipata maelezo kuhusu ubora wa sabuni na vipodozi vyao.
Na Richard Mwaikenda, Zanzibar
WAJUMBE wa Kamati ya Uongozi na watendaji wa Mpango wa Kurasimisha Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), wametembelea kikundi cha Zaidat Products Zanzibar wanufaika wa mpango huo wanaotengeneza aina mbalimbali za sabuni na vipodozi vya asili.
Baadhi ya sabuni wanazotengeneza katika kiwanda chao kilichopo Chukwaani, Unguja Zanzibar ni; ya mchele, kahawa, mkaratusi, mwani, tangawizi pamoja na vipodozi vyake.Wajumbe wa Mkurabita walifurahishwa na uzalishaji wa bidhaa hizo za asili huku wengine wakinunua kwa matumizi yao binafsi.
Mdau unaoombwa uendelee kusikiliza kupitia kwenye clip hii ya video ujue yaliyojiri wakati wajumbe walipotembelea kiwanda hicho cha wajasiriamali...
Imeandaliwa na;
Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
Nitazipataje hizi sabuni kilimanjaro
ReplyDelete