Hatua hiyo ya UNICEF inafuatia taarifa ya kupatikana kwa mgonjwa mpya wa Ebola kwenye mji wa Butembo jimboni Kivu Kaskazini, eneo ambalo lilikuwa kitovu cha mlipuko wa 10 wa ugonjwa huo uliotangazwa kumalizika mwezi Juni mwaka jana.
Taarifa ya Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) imeeleza kuwa, tayari wafanyakazi wa UNICEF kutoka ofisi ya Beni, wamefika Butembo kusaidia na kitengo cha afya mjini humo wakati huu ambapo Shirika la Afya Duniani (WHO) nalo pia likiwa limeshachukua hatua za kupeleka wataalamu wake kwa ajili ya kubaini watu waliokuwa karibu na marehemu aliyeaga dunia kwa Ebola.
Mlipuko wa 10 wa Ebola nchini DRC ulidumu kwa takribani miaka miwili na ulikuwa mlipuko wa pili kwa ukubwa duniani ukiwa na wagonjwa 3481 ambapo kati yao hao 2299 walifariki dunia na 1162 walipona.
Harakati za kukabili mlipuko huo zilikuwa zinakumbwa na changamoto kutokana na ukosefu wa usalama kwenye eneo hilo.
Ikumbukwe kuwa, mripuko mkubwa zaidi wa ugonjwa hatari wa Ebola ulitokea baina ya Disemba 2013 na Aprili 2016 na kuua zaidi ya watu 11,000 katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone huko magharibi mwa bara la Afrika.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇