Jumatatu, Feb 08, 2021
Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Mhe Omary Kumbilamoto leo amefanya ziara yake ya kikazi katika Kata ya Zingiziwa kutembelea Ujenzi wa Zahanati ya Zogoali ambayo ipo katika hatua za mwisho ili kuanza kutoa huduma kwa Wananchi.
Katika Ziara hiyo Mstahiki Meya aliambatana na Mganga Mkuu Manispaa ya Ilala Bi. Emily Lihawa pamoja na Diwani wa Kata ya Zingiziwa Mhe. Maige Maganga.
Lengo la ziara yake ni kuangalia changamoto ya Maji pamoja na umeme ambazo zimesababisha kituo hicho kuchelewa kutoa huduma. Kwasasa Tanesco wamekamilisha hatua zote za uingizaji wa Umeme katika Zahanati hiyo na muda wowote kutoka sasa Umeme utawaka.
Changamoto pekee iliyobaki amabayo Mstahiki Meya ameibeba na kuahidi kwenda kuifanyia kazi ni kisima cha maji safi kwaajili ya matumizi ya Zahanati.
Mganga Mkuu wa Manispaa Bi Emily Lihawa ameeleza kuwa changamoto kubwa iliyo bakia ni hiyo ya Maji lakini pia kuanzia sasa wanaanza kuingiza vifaa kwaajili ya kuanza kutoa huduma.
Bi Emily aliendelea kwa kueleza mpango wa Serikali katika kukarabati Zahanati ya Zingiziwa, Serikali Imetenga kiasi cha shilingi Mil 100 kwa ajili ya ukarabati wa Zahanati hiyo lakini pia Amewasilisha ombi kwa Mkurugenzi kusaidia Ujenzi wa Zahanati, Ujenzi huwo umeanza kwa nguvu za Wananchi katika Mtaa wa Nzasa.
Mwisho Mstahiki Meya alitembelea Daraja la kowa mbili, Lubakaja Shule ya Msingi pamoja na Kivuko cha kwa Mama Yusuph na kuahidi kuja na Engineer ili kuviingiza katika bajeji ya mwaka huu wa fedha.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇