Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
NAIBU waziri wa mifugo na uvuvi ,Pauline Gekul ,amemsimamisha kazi msimamizi Gabriel Liakulwa wa kituo cha ukaguzi wa mifugo kijiji cha Ruvu Darajani ,na kupisha uchunguzi baada ya kudaiwa kujinufaisha kupitia kituo hicho,huku akisababishia upotevu wa fedha za Serikali.
Aidha amempa salamu meneja wa Ranchi ya Ruvu na wafanyakazi wa Ranchi hiyo wajitathmini na kuacha njia fupi kujipatia fedha.
Alitoa maagizo hayo ,katika ziara ya mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo na Naibu Waziri huyo katika halmashauri ya Chalinze ,Bagamoyo.
Pauline alieleza ,wamebaini mambo yanayofanyika katika minada hivyo mtumishi huyu asimame apishe uchunguzi asicheze na maduhuli ya serikali.
“Maduhuli yanapotea kwasababu ya kufanya michezo ya wizi tutaendelea kusafiri na wakuu wa mkoa wanaofichua maovu kama mkuu huyu wa mkoa wa Pwani ,ambae amefichua wizi huu.
“Mtupishe ,tumechoka kutorosha mifugo na hatutovumilia,ondokeni hamtutoshi ,na mkuu wa mkoa usichoke kutuletea kama haya,”;alifafanua Pauline .
Pamoja na hayo ,Pauline amewaelekeza , maafisa ardhi na kamati za mipango miji katika halmashauri ya Chalinze wajipime kama wanatosha kwa kudaiwa kukalia migogoro ya muda mrefu bila kuitatua ikiwemo mpaka kati ya kijiji cha Chamakweza na kijiji cha Pingo.
Alieleza,mgogoro wa miaka takriban 20 Chamakweza na Pingo walipaswa kutoa majibu kwa wananchi pasipo kupoteza muda hadi sasa.
Aliwaasa wananchi kuvuta subira wakati serikali ikiendelea na michakato ya maamuzi.
“Heshimuni mipaka ,tulieni isipokuwa serikali ikitoa maamuzi hatutotaka mgombane ama kukinzana na maamuzi hatakayotolewa “
“Kila upande uheshimu upande mwingine ,kila mmoja ana shughuli yake kujiongezea kipato
Awali Ndikilo alifichua uozo uliopo katika kituo hicho kwa kusema kinatuhumiwa kuingiza ngombe kwa njia za Panya kwa gharama ya sh.milioni moja.
L
Aliwataja wananchi wanaohusika na mtandao huo ni Alex wa kijiji cha Ruvu Darajani na Bernard kijiji cha Nzoka pamoja na mchora ramani anaitwa Festo na msimamizi wa kituo Gabriel Liakulwa ambapo pia baadhi ya askari wanadaiwa kujiingiza katika hilo na Hamza Chibuma afisa mifugo .
Hata hivyo ,Ndikilo alimuagiza mkurugenzi ,kumsimamisha kazi ofisa mifugo was halmashauri Hamza Chibuma na mtendaji wa kijiji cha Ruvu Darajani ili kujiridhisha na uchunguzi .
Nae mtumishi Gabriel alikana kuhusika na tuhuma hizo na kusema kwasasa kuna utaratibu wa kukagua magari hayo kwa masaa 24 ,na wanatoa ulinzi.
Mbunge wa Chalinze ,Ridhiwani Kikwete alisema ,hiki kituo ni kama chanzo cha mapato cha halmashauri ya Chalinze lakini kituo hiki kimegeuzwa kuwa shamba la bibi.
Alieleza kijiji cha Kidogozero na Kitonga wanalalamika kero ya mifugo holela na wingi wa mifugo katika Ranchi ya Ruvu na ukiuliza inatokea wapi inadaiwa kutokea katika kituo hicho .
Ridhiwani alifafanua ,jambo hili ni la kweli na kilio hiki ni kikubwa .
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇