Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Dorothy Gwajima akizungumza alipotembelea banda la Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Bungemba, Mufindi ambao wamewashawishi wananchi kulima kilimo cha parachichi kujiongezea kipato wakati wa maonesho yanayoenda sambamba na mkutano mkuu wa Watalaamu wa Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma. Kulia ni Mhadhiri na Mratibu wa Ushirikishwaji wa chuo hicho, Raphael Mbiiji na kushoto ni Mwanafunzi wa chuo hicho, Theofrida Mwakalile. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDAWaziri Dk. Gwajima akikabidhiwa zawadi ya kuku na Mwenyekiti wa Kikundi cha Tusumuke, Christopher Dionizi kinachojishughulisha na ufugaji wa kuku jijini Dodoma baada ya kukopeshwa na halmashauri chini ya usimamizi wa maafisa wa maendeleo ya jamii.
Waziri Gwajima akipata maelezo kutoka kwa Benjamini Ndahani kuhusu kikundi cha vijana cha Kalalu Furniture kinavyoendesha shughuli zake za useremala baada ya kupata mkopo kutoka halmashauri. Kikundi hicho kipo Kata ya Uhuru jijini Dodoma.
Dk. Gwajima akiangalia nyaraka alipotembelea banda la Chama cha Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) wakati wa maonesho hayo yaliyowashirikisha vijana, wanawake na wenye ulemavu wanaonufaika na mikopo ya asilimia 10 itokanayo na mapato ya halamashauri nchini.
Waziri Gwajima akiondoka baada ya kutembelea maonesho hayo yanayofanyika nje ya Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Zaidi ya sh. bil. 23 zimekopeshwa kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu nchini. Walionufaika hadi sasa ni 6859.
Your Ad Spot
Feb 24, 2021
DK GWAJIMA AFURAHISHWA NA MAONESHO YA WANUFAIKA WA MIKOPO YA HALMASHAURI
Tags
featured#
KIJAMII#
Share This
About Richard Mwaikenda
KIJAMII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇