Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, akizungumza jijini Dodoma, kuhusu Maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwake ambapo wameamua kushirikisha jumuiza zake kuadhumisha kwa kupanda miti zaidi ya 150,000 pamoja na kufanya usafi nchi nzima.
Pia amesema katika kilele cha maadhimisho hayo kutakuwa na maonesho yenye lengo la kuelezea historia sahihi ya chama hicho kikongwe nchini yatakayofanyika White House jijini Dodoma Jumamosi Februali 6, 2021. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Raymond Mwangwala na kulia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT), Queen Mlozi.
Kushoto kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Raymond Mwangwala, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT), Queen Mlozi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi wa CCM, Erasto Sima. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDAKwa habari zaidi endelea kusikiliza clip hii ya video aliyozungumza Humprey Polepole jijini Dodoma...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇