Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita, Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay akikabidhi Hati za Hakimiliki za Kimila kwa wananchi wa Kijiji cha Lugodalutali wilayani Mufindi ambapo wananchi 342 walipata.
Wananchi wa Lugodalutali wakicheza kwa furaha wakati wa hafla ya kukabidhiwa Hati za Hakimiliki za kimila kulikofanywa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita, Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay wilayani Mufindi, Iringa Januari 25,2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halashauri ya Wilaya ya Mufindi, Netho Ndilito akizungumza wakati wa sherehe hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita, Immaculata Senje akijitambulisha wakati sherehe hiyo.
Mratibu wa Mkurabita, CPA, Dkt. Seraphia akizungumza maneno ya utangulizi kabla ya kukaribishwa Mwenyekiti wa Bodi, Balozi mstaafu, Njoolay kuzungumza na kugawa vyeti kwa walengwa.
Mmoja wa wanufaika wa Mkurabita, Fox akielezea jinsi aliokopa benki sh. mil. 150 kwa kutumia Hati za Hakimiliki na kupanua wigo wa biashara zake.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William akielezea mafanikio ya mradi huo wa urasimishaji mali za wanyonge uliofanwa kwa ushirikiano na Mkurabita kwa wakazi wa Kijiji cha Lugodalutali.
Baadhi ya watumishi wa Mkurabita wakaiwa katika sherehe hizo.
Na Richard Mwaikenda, Mufindi
WANANCHI 342 wa Kijiji cha Lugodalutali, wilayani Mufindi wamekabidhiwa na Mpango wa Urasimishaji wa Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) Hati za Hakimiliki.
Hakimiliki hizo zimekabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita, Balozi mstaafu, Daniel Ole Njoolay katika sherehe iliyofanyika Januari 25, 2021 katika kijiji hicho kilichopo Kata ya Igombavanu.
Wakikabidhiwa hakimiliki hizo zilizoandaliwa na Idara ya ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, wananchi hao walionesha furaha ya aina yake huku wakicheza kwa furaha ngoma yao ya asili.
Katika risara yao waliishukuru Mkurabita na serikali ya wilaya ya Mufindi kwa kuwapatia hakimiliki hizo ambapo walitaja mafanikio waliyoyapata na jinsi watakavyonufaika nazo.
Walitaja mafanikio watakayoyapata kuwa ni; Urahisi wa kupata dhamana ya mkopo katika taasisi za kifedha kama vile benki, kuwa wamiliki halali wa kiwanja na kutambuliwa rasmi,itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi baina yao na vijiji vingine pia makundi ya wakulima na wafugaji.
Akizungumza wakati wa sherehe hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi, Netho Ndilito alisema kuwa hayo yote ni matokeo kwani,Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ni moja kati ya Halmashauri za mwanzo zilizopewa kipaumbele katika mwaka 2011/2012 mkoani Iringa kwa kujengewa uwezo na Ofisi ya Rais-Mkurabita kwa ajili ya utekelezaji wa urasimishaji ardhi vijijini na kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia rasilimali wanazozimiliki.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William alisema kuwa kupitia hati hizo watapata fedha kwa kukopa benki ili wapate fedha za kuboresha maisha yao pamoja na kijiji hicho kuinuka kiuchumi.
"Hizo zote ni fursa ambazo serikali imeziweka ili wananchi mwuondokane na umasikini msonge mbele kimaisha, hiyo ndo kazi ya serikali kuwawekea mazingira mazuri kama ya Mpango wa Mkurabita, si kazi ya kuwawekea fedha mifukoni," alisema Mkuu wa wiaya.
Mratibu wa Mkurabita, CPA,Dkt. Seraphia Mgembe aliwataka waliopata hati hizo wasiogope kwenda kukopa fedha benki kwani zipo kwa ajili yao na endapo kuna wasioelewa mambo ya benki, amewashauri waende ofisi za wilaya kitengo cha maendeleo ya jamii wakasaidiwe.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita amewapongeza viongozi wa Kijiji hicho cha Lugodalutali na wilaya kwa kuwahamasisha wananchi kuhusu mkurabita na suala zima la maendeleo.
"Mnajua Mimi nimefanya kazi ya ukuu wa mikoa kwa miaka 16 hivyo kwa ikifika mahali hainichukui muda kuona hawa viongozi wameshikamana wanaongea lugha na wako timu moja, nawapongeza sana,"alisema Njoolay huku akishangiliwa na umati wa wananchi.
Baada ya kumaliza kuzungumza, Njoolay aliwakabidhi wananchi hao hati za hakimiliki huku akisaidiana na baadhi ya maafisa wa Idara ya Ardhi ya wilaya.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇