Na Richard Mwaikenda, Njombe.
KAMATI ya Uongozi ya Mpango wa Urasimishaji Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) pamoja na watendaji wa mpango huo, leo Januari 28, 2021, wametembelea maporomoko ya Mto Ruhuji mkoani Njombe.
Katika utalii huo wa ndani Kamati hiyo ya uongozi iliongozwa na Mratibu wa Mkurabita, Dkt. Seraphia Mgembe (aliyevaa sketi ya njano) ambapo yeye na jopo zima licha ya kufurahia kuona maajabu hayo, lakini wengi wao walionekana kuyashangaa maporomoko hayo yaliyopo micha chache kushoto unapoingia Mji wa Njombe ukitokea Makambako.
Walishuhudia baadhi ya wenyeji wakiogelea katika kwenye mabwawa yaliyojitengeneza chini ya maporomoko hayo, jambo ambalo pia liliwavutia kiasi cha baadhi yao kutamani kwenda kuoga lakini haikuwezekana kutokana na kukosa nguo za kuogelea.
Hivi karibuni Timu ya Watalaamu wa Serikali imefika na kufanya ukaguzi wa katika maporomoko ya Mto Ruhuji katika Kijiji cha Itipula mkoani Njombe ambao unatarajiwa kujengwa mradi mkubwa wa umeme wenye uwezo wa kuzalisha megawats 358 za umeme.
Mradi huo ambao utajengwa katika kipindi cha miezi 36 unaotarajiwa kuanza mwezi juni au julai mwaka huu.Ulifanyiwa utafiti kwa mara ya kwanza 1998 na kisha kusimama kwa muda mrefu jambo ambalo lilisababisha wananchi kupoteza matumaini na kuanza kurudi kwenye maeneo waliotakiwa kupisha.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mkurabita, Mujungu Masyenene akionesha maporomoko ya Mto Ruhuji.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Mhariri Mkuu wa Blog hii, Richard Mwaikenda na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mkurabita, Mujungu wakifurahi baada ya kuyaona maporomoko hayo.Picha na Abdul Maliki.
Baadhi ya wajumbe wakiangalia maporomoko hayo
Mtendaji wa Mkurabita, Asteria hakusita kupiga picha ya kumbukumbu ya maporomoko hayo.
Imeandaliwa na;Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇