Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akizungumza katika Mkutano wa Hadhara wa Rais Dk. John Magufuli katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, jana.
CCM Blog, Tabora
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ameeleza kwa undani umuhimu wa mkoa wa Tabora kihistoria, ikiwa ni pamoja na namna Mwalimu Nyerere alivyotoa machozi akipigania Uhuru wa Tanganyika mwaka 1958 akiwa mkoani humo.
Ameeleza hayo, jana, Januari 30, 2021 akiwa katika mkutano wa hadhara wa Rais na Mwenyekiti wa CCM Dk. John Magufuli uliofanyika katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
"Mkutano wa TANU uliofanyika hapa Tabora ulimtoa machozi Baba Wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere baada ya kutoa kauli na kusema kuwa kama Waingereza watachelewesha Uhuru, Watanganyika tutawashitaki kwa Malkia wao, Wasimpomtii, tutawashitaki Umoja wa Mataifa Wasipotii tutawashitaki kwa Mwenyezi Mungu", alisema Dk. Bashiru.
Pia Katibu Mkuu alielezea kwa undani na umuhimu wa namna ambavyo maelekezo ya Rais Dk. Magufuli ya kutilia mkazo somo la historia itakavyosaida kukuza uzalendo wa vijana kwa taifa lao.
Tafadhali msikilize kwa kina Dk. Bashiru katika video hii, Bofya Hapo👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇