LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 10, 2021

SHIRIKA LA AGRI THAMANI LIMEWATAKA MADIWANI WA HALMASHAURI MULEBA KUBEBA AGENDA YA LISHE KWENYE MAENEO YAO


MKURUGENZI wa Shirika la Agri Thamani Mhe Neema Lugangira (MB) akiwasilisha mada ya lishe kwenye semina ya Madiwani wa Halmashauri ya Muleba
iliyoandaliwa na Shirika hilo

MGANGA
Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Modest aliwasilisha mada ya Lishe kwa
Madiwani hao ambapo semina hiyo iliandaliwa na Shirikala Agri Thamani


MWENYEKITI wa Halmashauri ya Muleba Emmanuel Sherembi


Baadhi ya Madiwani wa wilaya ya Muleba wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye semina

MRATIBU wa Lishe kutoka Tamisemi Mwita Waibe na Mganga Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt Modest Mganga wakifurahia namna ambavyo semina ya Lishe imeendeshwa

MKURUGENZI wa Shirika la Agri Thamani Mh Neema Lugangira (MB) akigawa nakala mada kwa madiwani  iliyokuwa inawasilishwa na Idara ya Afya ya Halmashauri ya Muleba


 

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Agri Thamani Foundation limewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera kuendelea kubeba ajenda ya lishe kwenye maeneo yao ili kuweza kudhibiti hali ya udumavu katika wilaya hiyo.


Semina hiyo imewafikia Madiwani wa Kata ,Madiwani wa Viti Maalumu kutoka Kata zote 43 za wilaya ya Muleba.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa AgriThamani Foundation ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Tanzania Bara anayewakilisha Asasi za Kiraia (NGOs) Mhe. Neema Lugangira (Mb.)  wakati akizungumza na Madiwani, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Wakuu wa Idara wa Wilaya ya Muleba wakati wa Semina ya Lishe iliyoandaliwa na Agri Thamani. 


Amesema kuwa ili kupunguza udumavu katika wilaya ya Muleba ni kuhakikisha wananchi wanajikita katika mazao lishe pamoja na viongozi hao kushirikiana na watalaam wa lishe na kilimo ili kwenye vikao vya ngazi zao kuweza kutoa elimu iliyosahihi. 


Mbunge Neema Lugangira ameongeza kuwa viongozi hao wanatakiwa kushirikiana na watalam wa afya kutoa tathimini ya mara kwa mara kuhusu hali ya lishe kwenye maeneo yao kwani watalam hao hawawezi kuingia sehemu zote kwa wakati mmoja.


“Sisi sote tuna jukumu la kujua hali ya lishe, udumavu n.k. tunapaswa kuangalia katika mtaa wetu, katika kijiji chetu hali ikoje ya lishe na tukikumbana na hali ya  lishe duni na viashiria vyake tunatoa taarifa kwa wenzetu upande wa serikali” Alisema Mhe Neema Lugangira (Mb.)


Naye kwa upande wake,Mratibu wa Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mwita Waibe aliwaambia Madiwani kuwa Tamisemi imekuwa ikishirikiana na Agri Thamani kwa karibu huku akilipongeza Shirika hilo kutokana na kwamba ni NGO ambayo inafanya kazi za jamii na kuzifikisha ngazi ya jamii. 


Mratibu Mwita aliwasisitizia madiwani wa Halmashauri hiyo waendelee kuyatafsiri mafunzo haya kwa vitendo ili Agri  Thamani iweze kupata msingi wa kuandaa Programu zitazoshuka hadi ngazi ya vijiji. 


Kwa upande mwingine, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Muleba Agnes Kassela aliwataka Madiwani wa Halimashauri ya Wilaya ya Muleba kwa kutekeleza maagizo hayo kuhusiana na Ajenda nzima ya Lishe kama ilivyo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025  kwani sasa ni muda wa utekelezaji na wao ndio wasimamizi wakuu wa miradi ya maendeleo. 


Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Halamshauri ya Muleba Bwana Justus Magongo ameiliishukuru Shirika la  Agri Thamani kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Madiwani kwa kuwapatia elimu hiyo ya lishe ambayo ni muhimu sana. 


Alisema watahakikisha wanabeba ajenda ya lishe kwa vitendo kwenye Halmashauri hiyo kupitia vikao vyao na mipango kazi ili kuweza kupunguza kiwango cha udumavu katika Wilaya hiyo.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages