Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Binilith Mahenge akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao cha umoja wa taasisi tano zilizokubaliana kufanya kazi kwa ushirikiano kuharakisha maendeleo ya Mkoa wa Dodoma Januari 15,2021, jijini Dodoma .
RC Mahenge (katikati), akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Josephat Maganga (kulia) na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru baada ya kumalizika kwa kikao hicho cha pamoja.
Baadhi ya maofisa kutoka taasisi 5 zilizounda umoja wakiwa katika kikao hicho.
Afisa Mipango Jiji wa Hamashauri ya Jiji la Dodoma, Aisha Masanja akiwasilisha taarifa ya mpango mkakati wa kuliendeleza jiji hilo wakati wa kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru akifafanua jambo kuhusu mipango ya kuliendeleza jiji hilo.
Meneja wa Mkoa wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Dodoma, Frank Chambua akiwasilisha taarifa ya mipango ya kuboresha miundominu ya umeme katika jiji hilo.
Mratibu wa Wakala wa Barabara Vijijini (Tarura), Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Lusako Kilembe akiwasilisha kwenye kikao hicho taarifa ya mipango ya kuboresha miundominu ya barabara katika jiji la Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Usanifu na Ujenzi cha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), akiwasilisha taarifa ya jinsi ya kuboresha miundombinu ya maji Dodoma.
Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA), Dodoma Jiji, Michael Nguruwe, akiwasilisha mikakati ya uboreshaji wa miradi ya maji.
Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Happiness Mgalula akisoma maazimio ya pamoja ya kikao hicho kwa masuala yatakayopewa kipaumbele kuyatekeleza. Kulia ni Mhandisi wa Matengenezo Tanroads, Salome Kabunda.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, DK. Binilith Mahenge, ameunda umoja wa taasisi 5 za Serikali kufanya kazi kwa kushirikiana kuiletea Dodoma maendeleo ya haraka.
Dk. Mahenge amezikutanisha taasisi hizo katika kikao kilichofana kilichofanyika Januari 15, 2021 ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa Dodoma.
Taasisi alizokutano nazo ni; Wakala wa Barabara Vijijini, TATURA, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS),, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Duwasa), Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA), Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TanescoU.
Katika kikao hicho walizijadili taarifa za mipango mikakati zilizowasilishwa na taasisi hizo kuhusu miradi inayoweza kutekelezwa kwa ushirikiano kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya Jiji la Dodoma.
Mambo makubwa yaliyojadiliwa ni uboreshaji wa miundombinu ya Maji, Barabara na umeme.
Dk. Mahenge aliwapongeza wakuu wa taasisi hizo kwa kuandaa taarifa nzuri zilizojaa Mipango na.mikakati mizuri ya.kuiletea Dodoma.
Umoja huo umekubaliana kuwa na vikao kila baada ya miezi mitatu kupanga mikakati na utekelezaji wa miradi muhimu kwa jamii na maendeleo ikiwemo kuweka mazingira mazuri maeneo ya uwekezaji kwa kuandaa miundombinu ya barabara, umeme na maji kabla ili anayetaka kuwekeza aikute.
Miradi ya vipaumbele itawekwa msukumo wa pamoja na hata kushirikiana kwa hali na mali kuikamilisha.
Wakuu wa taasisi hizo wameupongeza utaratibu huo uioanzishwa na Dk. Mahenge na kuomba uendelee kwa faida ya maendeleo ya mkoa huo. Awali kila taasisi ilikuwa inafanya kazi kivyake jambo ambalo lilikuwa likichelewesha maendeleo.
Ili kuufanya umoja huo uendelee kuwa hai, imeundwa Sekretarieti ya kuratibu na kupanga kalenda ya vikao itakayokuwa na wajumbe kutoka kila taasisi pamoja na ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu wa Mkoa wa Ddodoma, Mhandisi Happiness Mgalula, alitaja aadhi ya maazimio ya kikao hicho kuwa ni;
Upembuzi na upimaji wa maeneo wainishe maneo ya kimkakati nan uwekezaji yatakayopewa kipaumbele.
Jiji la Dodoma lianishe maeneo matatu ya kipaumbele maeneo ya uwekezaji pia wafanye tathmini ya jinsi ya kuvuna maji ya mvua kupitia kwenye majengo na kuyaingiza kwenye mfumo,lakini pia watafute na kutambua visima vya watu binafsi.
Tanesco ihakikishe maeneo ya kimkakati yatakayoanishwa yanapatiwa umeme na Tanroads wafuatilie wizarani kuhusu hifadhi ya barabara kama ni mita 60 au 80.
Duwasa wawasilishe mchanganuo wa visima vipya na uchangiaji wa maji kwa miezi 3, miezi 6 hadi mwaka.
Ndugu nakuomba uendelee kumsikiliza RC Mahenge akizungumzia umoja huo kupitia clip hii ya video....
RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇