Wakitoka kwa Mkurugenzi kuelekea kwa Mkuu wa wilaya.
Timu ikielekea Ofisi za Wilaya ya Mbarali kukutana na Mkuu wa Wilaya pamoja na wadau wanufaika wa Mkurabita.
Wakiwa kwenye kikao cha utambulisho ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune (kulia). Kushoto ni ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita, Balozi mstaafu Njoolay.
Balozi mstaafu Njoolay, akizungumza wakati wa kikao na wadau walionufaika kwa kujengewa uwezo na Mkurabita wilayani Mbarali. ambapo zaidi ya wananchi 988 wamekopa benki zaidi ya sh. bilioni 19 kwa kutumia Hati za Hakimiliki za Kimila kama dhamana.
Mratibu wa Mkurabita, CPA Dkt. Seraphia Mgembe akielezea jinsi alivyofurahishwa na wadau walivyochangamkia fursa ya kutumia kukopa benki kwa kutumia Hati za Hakimiliki wilayani Mbarali.
Ofisa Mikopo kutoka Benki ya NMB, akielezea walivyofanikisha wanufaika wa Mkurabita kupata mikopo kwenye benki hiyo ambapo hadi sasa 155 wameshakopa zaidi ya sh. bilioni 7.
Afisa Ardhi na Maliasili wa Wilaya ya Mbarali, Geofrey Mwaijobele akisoma taarifa ya wilaya kuhusu mafanikio ya urasimishaji wa rasilimali za wanyonge baada ya kujengewa uwezo na Mkurabita.
Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Gabriel Mfune akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Mkurabita na wadau walionufaika na mikopo kutumia hati za hakimiliki za kimila.
Baadhi ya watendaji wa Mkurabita
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Mfune akiwa na wajumbe na baadhi ya watendaji wa Mkurabita |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇