MKE wa Rais Mama Mariam Mwinyi akifafanua jambo, alipokuwa akizungumza na Vijana wa UVCCM, baada ya kupokea Matembezi yao ya Maadhimisho ya Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika Skuli ya Msingi Mwera, Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, leo.
MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM ambae pia ni Waziri wa Vijana Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Mwita Maulid, akizungumza na Vijana walioshiriki Matembezi hayo.
NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Mussa Haji Mussa akizungumza na kutowa maelezo ya Matembezi hayo ya Vijana wa UVCCM, kwa mgeni rasmin Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, kabla ya kumkaribisha kuzungumza katika hafla hiyo, katika viwanja vya Skuli ya Msingi Mwera.
MKE wa Rais Mama Mariam Mwinyi alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Mwera kuyapokea Matembezi ya Vijana wa UVCCM, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Hamida Mussa Khamis, wakielekea katika sehemu ilioandaliwa kwa ajili ya hafla hiyo.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Mohammed Rajab Soud alipowasili katika Viwanja vya Skuli ya Mwera kwa ajili ya kuyapokea Matembezi ya Vijana wa UVCCM na kuzungumza nao, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa UVCCM ambae pia ni Waziri wa Vijana Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Mwita Maulid. (Picha zote na Ikulu, Zanzibar).
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇