UONGOZI wa Kituo cha Afya cha Ndalambo, Wilaya ya Momba
mkoani Songwe, umekigeuza chumba cha kuhifadhia maiti kuwa stoo ya muda.
Kituko hicho cha kusikitisha kiligunduliwa hivi karibuni na Mbunge wa Jimbo la Momba,
Condester Sichalwe akiwa katika ziara ya kukagua miundombinu katika kituo hicho cha Afya.
Alipoingia kwenye chumba hicho cha kuhifadhia maiti
alishangaa kukuta kimejazwa mifuko ya saruji na vitu vingine visivyofaa kuwemo
humo.
Alipoona hivyo alimhoji Mganga Mkuu wa Kituo hicho kuhusu
kitendo hicho kisicho cha kistaarabu, kuwa endapo ajali ingetokea afe hata mtu mmoja, maiti wangeiweka wapi?!!!
, alijibu kirahisi kuwa wangeviondoa vitu hivyo.
Mazingira ya chumba hicho hayakuridhisha kwani hata kitanda
kilichomo humo kilikuwa kimegubikwa na mifuko ya saruji na takataka zingine
huku sinki likiwa na maji machafu yanayoonekana yamekaa kwa muda mrefu.
Mbunge Sichalwe alionekana kutopendezwa kabisa na hali
aliyoikuta kwenye chumba hicho, kiasi
cha kumjia juu Mganga Mkuu wa Kituo kwa kutokuwa makini na kazi yake.
Ndugu mdau kwa kisa hiki cha kustaajabisha naomba uendelee
kumsikiliza na kumuona Mbunge Sichalwe kupitia clip hii ya video jinsi alivyokerwa baada kukuta hali hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇