LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 5, 2021

ASILIMIA 18 YA WAMILIKI UCHUMI TANZANIA WAWEZESHWA NA MKURABITA KUKOPA ZAIDI YA TRILIONI 1



Makao Makuu ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali za Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) zilizopo Nane Nane, Nzuguni, jijini Dar es Salaam.

 Mratibu wa Mkurabita, Crpa, Dkt. Seraphia Mgembe (kushoto), akifurahia jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi  katika ofisi za mratibu huyo wakati Ndejembi alipokwenda kujitambulisha  Mkurabita Desemba 30, 2020. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA.



Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma.

 ASILIMIA 11 ya wamiliki wa shughuli za kiuchumi Tanzania Bara wamekopa kiasi cha shilingi Trilioni 1.8 kutoka SACCOs, Benki na Taasisi ndogo za fedha na  upande wa Zanzibar asilimia 6 wamekopa sh. Bilioni 12.

 

Mafanikio hayo kwa wananchi yamo kwenye taarifa iliyotolewa na Mratibu wa  Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Crpa, Dkt. Seraphia Mgembe aliyoisoma wakati Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi alipofanya ziara hivi karibuni ofisi za Mkurabita, jijini  Dodoma.

 

Dkt. Mgembe alisema hilo ni moja ya mafanikio ya Mkurabita kwa wananchi kwa mujibu wa taarifa ya tathmini ya sekta isiyo rasmi ya mwaka 2018.

 

Katika taarifa hiyo, Dkt. Mgembe alitaja mafanikio zaidi yaliyowezeshwa na Mkurabita kuwa ni; asiliamia  2 ya wamiliki wa majengo, asilimia 1 ya wamiliki wa mashamba na asilimia 1 ya wamiliki wa viwanja wa Tanzania wametumia rasilimali zao kukopa kiasi cha Shilingi trilioni 1.06 kutoka katika taasisi hizo za kifedha.

 

Aidha, alisema jumla ya migogoro 25,409 ya matumizi ya ardhi Tanzania ilitambuliwa ambapo asilimia 64 ya migogoro ilikuwa  kati ya wananchi kwa wananchi, mipaka ya kijiji na kijiji, wawekezaji na wananchi, maeneo ya hifadhi za taifa na vijiji na wafugaji na wakulima.

 

Alitaja mafanikio yaliyopatikana kwa Taifa zima kuwa ni; kuongezeka kwa mapato yatokanayo na leseni katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, kupungua kwa migogoro ya ardhi kati ya makundi mbalimbali yanayotumia ardhi ambayo sasa yanapata muda wa kufanya uzalishaji zaidi kuliko migogoro.

 

Mengine ni; kuongeza thamani ya ardhi na tija ya uzalishaji wamazao mbalimbali kutokana na kutekeleza mipango ya11 matumizi bora ya ardhi na hasa utekelezaji wa mipangokazi ya jamii inayoandaliwa wakati wa urasimishaji, kuongezeka kwa walipa kodi ambao wamerasimisha rasilimali ardhi na biashara.

 

Pia, alisema baadhi ya Halmashauri za Wilaya zilizojengewa uwezo zimeanza kutekeleza zenyewe urasimishaji katika maeneo yao na kufanya urasimishaji kuwa endelevu.

 

Vilevile Halmashauri za wilaya 25 zimetekeleza urasimishaji

ambapo jumla ya mashamba 20,274 yamepimwa na

kutoa hati za Hakimiliki za Kimila 14,665, hivyo kufanya

jumla ya mashamba yaliyopimwa kufikia 134,162.

 

Jambo lingine muhimu Mkurabita imechangia uwepo wa ajira takribani 43,224 zilisababishwa na tija iliyotokana na urasimishaji wa ardhi na biashara  ambapo 7,304 zimetokana na ardhi na 35,917 biashara.

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages