LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 18, 2021

MBUNGE ASENGA AKUTANA NA MAWAZIRI BUNGENI KUJADILI UTATUZI WA KERO KILOMBERO

 

Mbunge Abubakar Asenga Mbunge wa Jimbo la Kilombero akiwa na Waziri wa Maji, Juma Aweso (kulia) baada ya kujadili jinsi ya kutatua kero ya maji katika jimbo hilo.

Mhe Mbunge Abubakar Asenga Mbunge wa Jimbo la Kilombero akiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk. Leonard Chamuriho baada ya kujadiliana kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Barabaraya Ifakara-Kidatu. 


Mhe Mbunge Abubakar Asenga Mbunge wa Jimbo la Kilombero ambaye amewasili Jumapili Usiku Tar 17 Jan Mkoani  Dodoma kwa kwa ajili ya vikao vya Kamati za Bunge, ameamua kutafuta suluhu ya kero za barabara na maji kwa kukutana na mawaziri wanaohusika na sekta hizo.


Leo Jumatatu Tarehe 18 tayari Mhe Mbunge ameonana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk. Leonald Chamuriho kuendelea Kufuatilia ujenzi wa Barabara ya Ifakara-Kidatu ambapo leo Makubaliano katika vitu  vilivyo kwama yanatarajiwa kusainiwa.


Aidha, Mhe Mbunge alikutana na Waziri Wa Maji Mhe Juma Aweso na Katibu Mkuu Wizara ya Maji kufuatilia Mradi wa Maji wa Kiburubutu ambapo Utaratibu wa Ukandarasi Unaendelea.


Mhe Waziri ameahidi kutembelea Kilombero hivi Karibuni.



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages