LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 2, 2021

LAITI AMANI INGEKUWA INAUZWA MADUKANI, WATANZANIA TUNGEKUWA MATAJIRI-ASKOFU CHANDE+video

Askofu Evance Chande wa Kanisa la EAGT Nazaret, Ipagala, jijini Dodoma akiwa na baadhi ya viongozi wa kanisa hilo wakati wa ibada ya kuukaribisha mwaka mpya 2021 maalumu kwa ajili ya  kuliombea Taifa kuwa la amani na utulivu.


Askofu Chande akiwaombea watoto na vijana wakati wa ibada hiyo.

 

Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma.

AMANI ni tunu ya Taifa letu, inatakiwa ilindwe, haiuzwi dukani na laitI kama ingekuwa inauzwa watanzania tungekuwa matajiri.

 Hayo ni maneno ya Askofu Evance Chande wa Kanisa la EAGT Nazaret, Ipagala, jijini Dodoma, aliyoyatoa wakati wa ibada ya mwaka mpya 2021 ya kuliombea Taifa kuwa la amani na utulivu.

Akihubiri wakati wa ibada hiyo, Askofu Chande alisema kuwa Amani katika nchi haiji hivi hivi, bali inalindwa na inaasisiwa kutoka kwa viongozi walioliongoza Taifa kuanzia wakati wa Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Hayati Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete na sasa Rais John Magufuli.

Anasema kuwa amani ambayo ni tunu ya Taifa letu, inatakiwa ilindwe isichezewe na atakayejaribu kuichezea kwa kumficha adui wa taifa letu, asionewe  haya apigwe mawe kwa lengo la kuwaokoa watanzania walio wengi.

Katika ibada hiyo, pia aliwaombea watu wa makundi mbalimbali waliokuwepo kanisani na wasiokuwepo akianza na Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mawaziri, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, wabunge, wafanyabiashara, wakulima na wafugaji, wanafunzi, wajane na yatima pamoja na wanahabari.

Ndugu wadau mengi alihubiri katika ibada hiyo iliyotawaliwa na nderemo, vigelegele na shangwe za kumtukuza Mungu, hivyo naomba muendelee kumsikiliza Askofu Chande kupitia clip hii ya video....

IMEANDALIWA NA;
  RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages