Katibu Mkuu was UVCCMMwalimu Raymond (aliyevaa nguo za rangi ya Bluu), akishiriki kuomba Dua wakati was mazizi ya aliyekuwa mtumishi wa Jumuiya hiyo.
Ifakara , Morogoro
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa VIjana wa CCM ( UVCCM) Mwalimu Raymond Mwangwala (MNEC), ameongoza mazishi ya aliyekuwa mtumishi wa Umoja wa Vijana wa CCM Afisi ndogo ya Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar Haji Sultan Tembe maarufu kwa jina la (Haji Kaka) yaliofanyika Ifakara Mkoani Morogoro.
Wakati akitoa salamu za Jumuiya Katibu Mkuu alisema amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Haji kaka ambaye wiki iliyopita tu alikuwa naye Zanzibar katika matembezi na alikuwa naye akimpa majukumu ya Umoja wa Vijana ambayo aliyatekeleza kwa ufanisi mkubwa.
“Nilipopata taarifa hii ya kifo cha Haji kaka kwa kweli sikuamini nimeamua kusafiri kutoka Dodoma kuja mpaka hapa Ifakara kutaka kupata uhakika kama ni kweli mwezetu huyu ametutoka, na nilipofika hapa nimeamini na kushuhudia kuwa ni kweli Haji kaka hatunaye tena duniani “ Alisema kwa masikitiko makubwa
“Kitu kikubwa ni kumuombea mwenzetu huyu ambaye ametangulia mbele za haki, na sisi tuliyobaki duniani hii iwe kama darasa kwetu kikubwa ni kufanya ibada na kumuomba sana Mwenyezi Mungu kwa sababu kila mtu ataondoka katika dunia hii “ Alisema Katibu Mkuu, huku akiwapa pole watumishi na wana CCM wote waliotoka Zanzibar kwa moyo wao wa upendo na utu kuhakikisha wanamsindikiza ndugu Haji Kaka
“Kwa kweli Mwenyezi Mungu atawalipa wenzetu kutoka Zanzibar mlichokifanya ni kitu kikubwa sana na Mungu atawalipa tunawashukuru kwa kufanikisha mmefika mpaka ifakara na kumpumzisha mwenzetu Mungu awabariki sana” Alimaliza kuwashukuru.
Alkadhalika Katibu Mkuu Mwl.Raymond Mwangwala ambaye aliongoza ujumbe wa Jumuiya ya Vijana wa CCM kutoa pole kwa baba wa Marehemu aliwashukuru wana CCM wote wa KIlombero pamoja na wa Ifakara kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kuhakikisha Ndg.Haji Kaka anahifadhiwa katika nyumba yake ya Milele.
Katika tukio hilo walikuwepo pia Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali kutoka Kilombero na Ifakara ambao walijumuika kwa pamoja katika msiba huo.
Marehemu Haji Kaka alifariki tarehe 17 /01/2021 kwa matatizo ya kushindwa kupumua.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇