1.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya kushughulikia mgogoro wa Matumizi ya ardhi uliodumu kwa muda mrefu katika Kata ya Mtakuja, Mtaa wa Chang’ombe jijini Dodoma.
Na Eliafile Solla
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amepokea taarifa na mapendekezo ya utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika Kata ya Chang'ombe jijini Dodoma, alipokutana na Kamati iliyoundwa na Serikali kushughulikia mgogoro huo, leo.
Mgogoro huo wa matumizi ya ardhi yenye eneo la hekta kumi, baina ya wananchi na wananchi katika mtaa wa Mtakuja, Kata ya Chang’ombe umedumu kwa muda mrefu licha ya jitihada mbalimbali za Serikali za kuutafutia ufumbuzi.
Serikali iliunda kamati maalum ya kushughulikia mgogoro huo wa matumizi ya ardhi na baadae kuamua kupanga na kupima eneo hilo na kubadilisha matumizi kutoka yale ya awali na kuwa Makazi kutokana na uhalisia na maendelezo yaliyokwisha kufanyika kupitia mradi wa maboresho wa mwaka 2015.
Kamati hiyo imekutana na Waziri Lukuvi jijini Dodoma leo na kuwasilisha taarifa na mapendekezo yake jinsi ya kuushughulikia mgogoro huo ambapo Mhe. Waziri Lukuvi atatoa maagizo baada ya kuipitia taarifa hiyo na kujiridhisha.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇