Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imetunukiwa Tuzo na Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) kwa kutambua mchango wake katika sekta ya elimu nchini, wakati wa Mkutano Mkuu wa 15 wa chama hicho, uliofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma Desemba 21, 2020. Pichani Jafo akimkabidhi tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Uratibu wa Udahili na Utunzaji Kanzi Data wa TCU, Dkt. Kokuberwa Mollel. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo akihutuia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 15 wa Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA),
Wajumbe wa mkutano Mkuu wa TAHOSSA, wakipiga makofi baada ya kufurahishwa na hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (TAMISEMI), Seleman Jafo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Chama hicho.
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TAHOSSA.
Waziri wa Tamisemi, Jafo akizungumza jambo na Dkt Mollel pamoja na Afisa Udhibiti Ubora wa TCU, Mathay Mathang'a alipotembelea banda la TCU katika maonesho ya wadau wa sekta ya elimu yaliyofanyika sambamba na mkutano huo.
Waziri Jafo akikabidhiwa zawadi ya vitabu na kikombe
Waziri Jafo akizungumza na wanahabari baada kumaliza kutembelea mabanda.
Dkt. Mollel akizungumza na wanahabari kuhusu utendaji wa tume hiyo na jinsi walivyoshiriki kutoa mada na ushiriki wao katika maonesho hayo ya siku tatu.
SIKILIZA CLIP YA VIDEO HII UJUE ALICHOONGEA MKURUGENZI DKT MOLLEL.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇