LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 21, 2020

WAZIRI JAFO AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 15 WA CHAMA CHA WALIMU WAKUU WA SEKONDARI TANZANIA,TAHOSSA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo akihutubia  alipokuwa akiungua  Mkutano Mkuu wa 5 wa Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA), kwenye Ukumi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma Desemba 21, 2020. Taasisi ya Global Education Link (GEL) ndiyo waratibu wakuu na moja ya wadhamini wa mkutano huo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Waziri Jafo akisisitiza jamo alipokuwa akihutuia ambapo pia aliwaamia wajumbe salamu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli kuwa amefurahi sana uwepo wa mkutano huo muhimu na kuwashuuru waimu wakuu kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa mwaka mzima kusimamia suala la elimu kwa wafanafunzi kwa mwaka mzima na kwamba serikali itaendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha.

 

Naibu Katibu Mkuu OR TAMISEMI anayeshughulikia elimu Gerald Mweri akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 15 wa wakuu wa shule za Sekondari Tanzania TAHOSSA Mkutano unaofanyika kwa siku tatu Jijini Dodoma. 

Rais wa Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania TAHOSSA Mwalimu Frank Mahenge akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 15 wa wakuu wa shule za Sekondari Tanzania TAHOSSA Mkutano unaofanyika kwa siku tatu Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa TAHOSSA, akitoa neno la shukrani kwa niaa ya wajumbe baada ya Waziri Jafo kufungua rasmi mkutano huo wa siku tatu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akielezea jinsi mkutano huo alivyouratibu kwa kushirikisha wadau mbalimali wa sekta ya elimu kwa lengo la kufanikisha vizuri mkutano huo. GEL ni waratiu wakuu wa mkutano huo wa 15 na moja ya wadhamini. wa 
Wajume wa TAHOSSA wakipiga makofi baada ya kufurahishwa na hotuba ya Waziri Jafo.

Sehemu ya wajume wa mkutano huo amabao umehudhuriwa na walimu wakuu wa shule za sekondari  pamoja na wadau wa sekta ya elimu nchini.




Waziri Jaf akikabidhi tuzo kwa baadhi ya walimu wakuu  kwa kutambua mchango wao katika kuendeleza sekta ya elimu nchini.



Waziri wa Tamisemi, Jafo akikaidhi tuzo ya TAHOSSA kwa Mkurugenzi wa Uratibu na Udahili na Kutunza Kanzi Data wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU, Dkt. Kokuberwa Mollel  kwa kutambua mchango mkubwa wa tume hiyo wa kuendeleza sekta ya elimu nchini.Pia walishiriki kutoa mada pamoja na maonesho.

Waziri wa Tamisemi, Jafo akikaidhi tuzo ya TAHOSSA kwa Maofisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu  (HESLB) kwa kutambua mchango mkubwa wa Bodi hiyo wa kuendeleza sekta ya elimu nchini. Walitoa mada ya jinsi ya kuomba mkopo.

Waziri wa Tamisemi, Jafo akikabidhi tuzo ya TAHOSSA kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taaisi ya Global Education Link, Abdulmaliki Mollel  kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi  hiyo wa kuendeleza sekta ya elimu nchini. Taasisi hiyo  ni waratibu wakuu  wa mkutano huo wa 15 wa TAHOSSA.

Baadhi ya walimu wakuu waliopatiwa tuzo wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Tamisemi na viongozi wengine.
Wadau wa sekta ya elimu na wadhamini wa mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Tamisemi , Jafo na viongozi wengine.
Waziri Jafo akiondoka baada ya kutemelea mabanda ya maonesho ya wadau wa sekta ya elimu.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Education Link, Abdulmalik Mollel akizungumza na vyombo vya habari jinsi taasisi hiyo ilivyoratibu  kwa mafanikio makubwa mkutano mkuu wa 15 wa TAHOSSA kwa kuwashirikisha wadau mbalimali wa sekta ya elimu na afya.

SIKILIZA CLIP HII YA VIDEO MKURUGENZI MTENDAJI WA GLOBAL EDUCATION LINK,MOLLEL  AKIELEZEA MAFANIKIO YA MKUTANO HUO WA TAHOSSA.

IMEANDALIWA NA; 
RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI LOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages