LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 21, 2020

RWANDA YAONGEZA ASKARI WAKE AFRIKA YA KATI

 

Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya kati Faustin Archange Touadéra akisindikizwa na walinzi wa raia wa Rwanda na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa
Maelezo ya picha,

Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya kati Faustin Archange Touadéra akisindikizwa na walinzi wa raia wa Rwanda na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametangaza kwamba nchi yake iliamua kutuma askari katika Jamuhuri ya Afrika ya kati ili kulinda askari wa nchi hiyo waliomo katika kikosi cha umoja wa mataifa ambao wamekuwa wakilengwa na wanamgambo wenye silaha.

''Tulituma askari zaidi katika Jamuhuri ya Afrika ya kati kufuatia mapatano ya ushirikiano yaliyopo baina yetu na taifa hilo.... Majukumu ya askari hao na wengine waliopo katika kikosi cha umoja wa mataifa yatakuwa tofauti na yatatusaidia kulinda ama kuongeza nguvu za askari wetu ambao wamekuwa wakiviziwa na makundi yenye silaha na pia kulinda raia walioko katika sehemu mbali mbali zenye usalama mdogo'', amesema Kagame katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kigali.

Rwanda pamoja na serikali ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati wamemshutumu rais wa zamani wa nchi hiyo François Bozizé kwa kuwaunga mkono waasi na kupanga njama ya mapinduzi, shutuma ambazo alizikana.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa mashambulio ya waasi yamezimwa.

Vikosi vya Minusca pia vilepelekwa katika mji wa Bangui "kuzuia makundi yenye silaha ", AFP ilimnukuu msemaji wa Umoja wa Mataifa akisema.

Bw Kazagui pia amesema kuwa Rwanda imetuma mamia kadhaa ya wanajeshi ambao wamefika nchini humo na wameanza mapigano.

Paul Kagame
Maelezo ya picha,

Rais Paul Kagame anasema walituma askari zaidi ili kuwalinda askari wa Rwanda waliokua wakilengwa kwa mashambulio ya waaasi

Takriban wanajeshi 750 wa Rwanda na maafisa wa polisi wamekuwa wakifanyia kazi nchini humo chini ya kikosi cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa kinachojulikana kama Minusca.

Rwanda imepeleka kile inachokiiya "kikosi cha ulinzi " katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati baada ya walinzi wake wa amani kushambuliwa na waasi katika mji mkuu, Bangui.

Bw Bozizé amezuiwa kushiriki uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumapili.
Maelezo ya picha,

Bw Bozizé amezuiwa kushiriki uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumapili.

Rais Faustin Archange Touadéra amesisitiza kuwa uchaguzi wa Jumapili utaendelea kama ulivyopangwa, akisema kuwa uwepo wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa unamaanisha kuwa watu hawana la kuogopa.

Lakini vyama vya kisiasa vya upinzani, kikiwemo cha Bw Mr Bozizé, vimetoa wito wa kuahirishwa kwa uchaguzi "hadi amani na usalama vitakapopatikana ".

Makundi ya waasi yamechukua udhibiti wa miji kadhaa iliyopo karibu na mji mkuu Bangui , huku wakikabiliana na vikosi vya usalama na kupora mali, na Umoja wa Mataifa umeseam kuwa wanajeshi wake wanafanya hima kule amani Bangui.

Msemaji wa Bw Bozizé Christian Guenebem alisema : "Tunakanusha kabisa kwamba Bw Bozizé ni chanzo cha kila kitu ."

Wahusika wakuu katika mzozo ni akina nani?

Bw Bozizé, ambaye ni Mkristo, aliingia madarakani baada ya mapinduzi ya mwaka 2003 na akashinda uchaguzi ambao uliangaliwa na watu wengi kama uchaguzi uliotawaliwa na wizi wa kura. Alipinduliwa mwaka 2013 na wanamgambo wa Séléka - muungano wa waasi wa waislamu walio wachache -ambao unamshutumu kuvunja makubaliano ya amani.

Tangu wakati huo nchi hiyo imekumbwa na zozo baina ya vikosi vinavyoitwa Séléka na kinachoitwa "anti-Balaka" ambacho zaidi ni cha Wakristo.

Ni lipi tisho kwa sasa?

Jumapili , makundi mengine matatu makuu ya waasi yalitangaza kuwa wameunda muungano waliouita Patriots for Change (CPC), awakimshutumu Rais Touadéra kwa kujaribu kuiba kura katika uchaguzi ujao.

Katika taarifa yake CPC uliwaalika "makundi yote kujiunga nao " na wakaomba wajumbe wote "kuheshimu maadili ya raia ".

Huku kampeni za uchaguzi zikipamba moto, Facebook ilisema wiki iliyopita kuwa imebaini kampeni za upotoshaji ili kushawishi upigaji kura-uliopangwa na watu binafsi wenye uhusiano na jeshi la Ufaransa na mfanyabiashara maarufu wa Urusi Yevgeniy Prigozhin.

Urusi imetuma "mamia kadhaa ya wanajeshi na silaha nzito " nchini humo kuunga mkono serikali, shirika la habari la AFP limemnukuu msemaji wa serikali ya Jamuhuri ya Afrika ya kati akisema.

Moscow imeimarisha uhusiano wa karibu na Jamuhuri ya Afrika ya kati hivi karibuni . Washauri wa masuala ya kijeshi wa Urusi kwa sasa wako nchini humo kusaidia kutoa mafunzo vikosi vya serikali

Ripoti ya wachunguzi wa Umoaja wa Mataifa, jeshi la Marekani na Waandishi wa habari pia imebaini shughuli za kundi la Wagner Group, ambalo ni kampuni binafsi ya kijeshi inayodaiwa kumilikiwa na mrusi Bw Prigozhin.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages