MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC)Taifa anayewakilisha mkoa wa Iringa Salim Abri Asas amesema uchaguzi umekwisha ila wapo watu ambao bado wanaleta chokochoko ndani ya chama jambo ambalo si sahihi.
Asas ametoa kauli hiyo jana mjini Mafinga wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa CCM wilaya ya Mufindi .
Huku akitaka chama kuwachukua hatua kali wote wanaoendesha mifarakano ndani ya chama kuwa watu hao si wema ndani ya chama .
Kuwa umezuka mtindo wa watu kuchafua viongozi wa chama na serikali na kutaka watu hao wasifumbiwe macho wachukuliwe hatua kali .
“Hili jambo limekuwepo sana katika mkoa wa Iringa kwa watu hao wakishirikiana na wasio wana CCM kuchafua watu naomba watu hao wasifumbiwe macho kuna watu wananitumia jumbe za vitisho kuwa tutakuchafua wewe hebu mnichafue kwa ajili ya CCM sitishiki “alisema Asas
Kuwa chama kipo Imara na kitaendelea kuwa imara na hakuna kiongozi ama mwanachama atakayetishwa na watu hao .
Asas aliwataka wana CCM kutambua kuwa uchaguzi umekwisha na sasa ni wakati wa kufanya kazi na sio kushinda kwenye mitandao kutokana na kutisha watu.
Aidha Asas alimpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kumteua naibu waziri wa viwanda na biashara Exzaud kigahe kutoka jimbo la Mufindi Kaskazini na kuwa kutokana na majukumu ambayo naibu waziri huyo atakuwa nayo kwa upande wake atakuwa akimsaidia sehemu ya vitu kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya jimbo
“Ndugu zangu kuna kata vimefanya vizuri sana kwenye uchaguzi kwa kushinda kwa asilimia 100 kama kata ya Kihohela hawa naomba kuwajengea ofisi ya kisasa pia kata nyingine zote nitatoa zawadi ya 100,000 na siku za mbeleni basi kuwakarabatia ofisi zao “
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Daud Yassin akimkabidhi tuzo MNEC Salim Asas Leo
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Daud Yassin akimkaribisha Asas kufungua kikao cha Halmashauri kuu maalumu ya CCM wilaya ya Mufindi alisema chama kimeanza kuwachunguza wanachama wake 8 ambao hawakuwa na chama wakati wa kampeni na muda wote walikuwa wakitaka CCM ishindwe kwenye uchaguzi mkuu.
Alisema hawatamuonea mtu wasaliti wote wataitwa kujieleza kabla ya kuchukuliwa hatua kali .
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇