LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 18, 2020

DK. MAHENGE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA DODOMA (RCC)

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge  ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa huo (RCC),  akiongoza kikao cha kamati  hiyo cha kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo mkoani humo, Desemba 17, 2020. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), wakiwa katika kikao hicho muhimu  amacho kinafanyika mara mbili kwa mwaka. 




Mhifadhi Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),  Yohanes Sanga akitoa taarifa ya maazimio ya RCC.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa akiwaasa wajumbe kutekeleza kwa makini Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba hivi karibuni viongozi wa CCM wataanza ziara ya kufuatilia utekelezaji huo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chemba, Sambala Said akielezea umuhimu wa viongozi wa ngazi za juu kutembelea shule na kuongea na wanafunzi ikiwa ni moja ya mbinu ya kuwajengea uwezo wa kielimu na ufaulu mzuri.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo  akielezea  kuhusu mfumo wa kutambua rekodi za mapato kupitia mashine za kielectroniki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Mafuru akielezea jinsi jiji liliyyojipanga
 kuongeza mapato kupitia vitegauchumi mbalimbali vilivyoanzishwa na vitakavyoanzishwa

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Best Magoma akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na wajumbe kuhusu sekta ya afya
Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma,  Maria Lyimo akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na wajumbe
Munge wa  Chemba, Mohamed Monni akiuliza swali kuhusu vigezo vinavyotumika kusajiri shule.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi,Dk. Fatuma Mganga  akielezea mbinu na mikakati iliyotumika   kuifanya Bahi kuongoza kwa ufaulu wa wanafunzi kimkoa.

Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akishauri Mkoa kuwa na ajenda moja ya kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.
Baadhi ya wana sekretarieti ya RCC wakiwajibika
Wajumbe wa RCC wakifuatilia kwa makini mwenendo wa kikao hicho


Na Richard Mwaikenda, CCM Blog Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge  ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa huo (RCC),  ameongoza kikao cha kamati  hiyo ambacho kimejadili mambo mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.

Kamati hiyo ya ushauri inashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wakuu wa idara wa ofisi ya mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji wa halmashauri, wabunge, wenyeviti wa  halmashauri na baadhi ya viongozi wa taasisi.

Awali wajumbe walithibitisha  muhtasari wa mambo yote yaliyopitishwa katika kikao kilichofanyika mwaka jana Desemba 19, 2019

Katika kikao hicho  wajumbe walijadili  mada mbalimbali zilizowasilishwa za jinsi ya kuboresha sekta ya elimu, sekta ya afya, tathmini ya hali ya chakula na maandalizi ya kilimo msimu wa . 2020/21.

Pia, wajumbe walipitia  Mpango wa Bajeti ya mwaka  2019/20 na 2020/21 kufikia Noemba 2020,  Mpango wa Bajeti  wa mwaka  2019/20 kufikia Novemba 2020 na mwelekeo kwa mwaka 2021/22, mapato ya ndani ya Halmashauri na matumizi kufikia Novemba 2020.

Aidha,wajumbe walipatiwa taarifa  ya mwenendo wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani  Oktoba 2020, Taarifa ya utekelezaji wa  maazimio ya Kamati hiyo ya Wakala kwa Huduma ya Misitu (TFS).

Mkuu wa Mkoa, Dkt. Mahenge ameagiza TFS  kuweka utaratibu wa kukagua mara kwa mara mwenendo wa upandaji miti katika halamashauri zote ii kuifanya Dodoma kuwa ya kijani. Mkakati huo uhusishe viongozi wa ngazi zote, wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na viongozi wa mkoa.

Baadhi ya maagizo yaliyotolewa kwenye kikao ni; kuunda Kamati ya Mkoa ya kufuatilia uboreshaji wa  elimu ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa Mkoa huo ambao kwa hivi sasa unashika nafasi ya 22 kitaifa.

Dkt. Mahenge amewataka viongozi  wote  wajenge umoja na ushirikiano kwa kuweka misingi imara ya kudumu  ya kuinua kiwango cha elimu ambayo ni ufundishaji bora, usimamizi, ufuatliaji na utawala.

Halmashauri zimetakiwa kuandaa vivutio vya uwekezaji, kutenga maeneo maalumu ya uwekezaji  na kuangalia uwezekano wa kupunguza bei ya ardhi kwa wawekezaji na hata ikiwezekana kuingia ubia nao.

 

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages