LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 16, 2020

DK MAHENGE AZITAKA TARURA, TANROADS KUWASHIRIKISHA WANANCHI KABLA YA KUANZA UJENZI WA MIRADI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya mkoa huo, Dk. Binilith Mahenge akiongoza kikao cha Bodi ya Barabara ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe walipata taarifa za  maendeleo ya ujenzi wa  barabara  mkoani humo kutoka Tanroad na Tarura  Desemba 16, 2020 jijini Dodoma. 

Dk. Mahenge amezitaka Tarura na Tanroads kuwashirikisha wananchi wa maeneo  husika kwa kupata maoni na ushauri  wao kabla ya kuanza ujenzi wa barabara na madaraja katika maeneo yao ili kujenga miradi imara inayozingatia jiongrafia na historia ya eneo husika.    

 Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Happiness Mgalula akisoma ajenda za kikao hicho.


 Spika wa Bunge, ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai  akitoa hoja kuhusu umuhimu wa Miji midogo kama Kibaigwa  kutengewa na Tanroads fedha za ujenzi wa barabara na kupanua maeneo ya kuegesha magari yakiwemo malori  ili kupanua wigo wa kibiashara na kuongeza ajira kwa vijana katika eneo hilo. Ndugai pia ni mjumbe wa  bodi hiyo.


 Mratibu wa Wakala wa Barabara vijijini  (TARURA) Mkoa wa Dodoma, Mhandisi  Lusako Kilembe  akitoa taarifa kwenye kikao hicho kuhusu mipango ya utekelezaji  ya miradi ya barabara za  Tarura kufikia hadi Novemba, 2020.


 Mhandisi Mwandamizi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Mhandisi Jacob Mukasa akielezea katika kikao hicho , kuhusu manufaa na namna mfuko  unavyopanga vipaumbele vya kutoa fedha.

 Mhandisi wa Barabara wa Tanroads, Clement Ngirwa akielezea katika kikao hicho, kuhusu utaratibu wa kupandisha hadhi barabara na majukumu ya Kamati ya Kitaifa ya Kupanga Barabara katika Hadhi Stashiki.

Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde akichangia hoja akitaka uwepo utaratibu wa barabara za jamii nazo kutengea fedha kwa ajili ya matengenezo.

Mbunge wa Kondoa Vijijini, Dk. Ashatu Kijaji  akichangia hoja wakati wa kikao hicho kwa kuzitaka Tarura na Tanroads kuwa na watalaamu wenye ueledi ili waweze kujenga miradi imara kuiiko wanaojenga miradi ya barabara na madaraja dhaifu ambayo mvua ikinyesha  inabomoka kirahisi.

 Mbunge wa Chemba, Mohamed Monni, akichangia hoja wakati wa kikao hicho.

 Mkuu wa Wilaya ya Kondoa,  Sezaria Makota akichangia hoja wakati wa kikao hicho. Kuhoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dk. Fatuma Mganga na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda.

Baadhi ya wajumbe wakiwa katika kikao hicho

Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Salome Kabunda   akitoa taarifa kwenye kikao hicho kuhusu mipango ya utekelezaji  ya miradi ya barabara za  Tanroads hadi Novemba, 2020.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chemba,  ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi hiyo, Sambala Said  


 IMEANDALIWA NA
 RICHARD MWAIKENDA

MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM

0754264203



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages