LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 18, 2020

DK. HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA CCM MKOA WA KASKAZINI PEMBA, LEO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili na Mkewe Mama Maryam Mwinyi, katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba, kwa ajili ya kuzungumza na Viongozi wa CCM na Jumuiya za Chama na Mabalozi wa CCM  wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, leo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa risala ya Viongozi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba na Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskazini Khadija Hassan Abdi, wakati wa mkutano wake na Viongozi hao kutowa shukrani zake kwao, uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Wete Pemba leo

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuzungumza na Viongozi wa CCM na wa Jumuiya za Chama  na Mabalozi wa CCM wakati wa mkutano wake na Viongozi hao uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba.(Picha na Ikulu)


NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Sadala (Mabodi) akizungumza wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Hussein Ali Mwinyi na Viongozi wa CCM na Mabalozi uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba leo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Viongozi wa CCM wa Jumuiya za Chama na Mabalozi na kutowa shukrani zake kwao kwa kumchagua kuwa Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi oktoba 2020, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Wete, Pemba.

BAADHI ya Viongozi wa Jumuiya za Chama na Mabalozi wa CCM wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba leo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, akisalimiana na Mabalozi wa CCM wa Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya kumaliza mkutano wake uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba leo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages