Mkuu wa Chuo cha Ufundi Donbosco Dodoma, Father Boniface Mchami akigongea glasi baadhi ya waalikwa ikiwa ni ishara ya kutakiana heri wakati wa kongamano maalumu la viongozi wa taasisi zinazoajiri vijana wanaofuzu chuoni
hapo lililofanyika chuoni hapo Desemba 4,
2020 jijini Dodoma.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Wageni waalikwa wakitakiana heri kwa kugongeana glasi
Baadhi ya wageni waalikwa wakigongeana glasi kutakiana heri
Mshauri wa Wanafunzi wa chuo hico, ambaye pia alikuwa msereheshaji Anancia Lema akiendelea na kazi yake
Father Boniface akijadiliana jambo na baadhi ya wageni waalikwa
Meneja Masoko wa chuo hicho, Deo John akielezea mikakati mbalimbali iliyopangwa na uongozi ya kukiboresha chuo, |
Waajiri na wageni waalikwa wakiwa kwenye majadiliano kutoa ushauri wa kukiwezesha chuo hicho kusonga mbele kimaendeleo.
Oswald Manyerere
Kozi hiyo imetangazwa na Mkuu wa Chuo hicho, Father Boniface Mchami wakati wa kongamano maalumu la viongozi wa taasisi zinazoajiri vijana wanaofuzu chuoni hapo lililofanyika chuoni hapo Desemba 4, 2020 jijini Dodoma.
Akizungumza katika kongamano hilo, Father Boniface , alisema maandalizi ya kozi hiyo yamekamilika kwani hata baadhi ya vifaa vya kufundishia tayari vimewasili nchini kutoka nje wakiwemo watalaamu.
Father Boniface ambaye pia ni Mkurugenzi wa Donbosco Dodoma, amesema pamoja na mambo mengine kozi hiyo itakuwa inafundisha masuala ya ya kilimo cha umwagiliaji na Kitalu Nyumba (Green House) ili kupata mazao bora.
Katika kongamano hilo lililoambatana na chakula cha usiku, wageni waalikwa ambao ndiyo waajiri wa vijana wanaofuzu chuoni hapo, walipata wasaa wa kushiriki majadiliano ya jinsi ya kukiboresha chuo hicho.
Wengi walikimwagia sifa lukuki chuo hicho kwa kuzalisha vijana wenye ujuzi , nidhamu ya hali ya juu na wanaofuata maadili kiasi cha kutojuta kuwapatia ajira.
Waliushauri
uongozi wa chuo kuongeza jitihada za
kukitangaza zaidi chuo hicho ili kijulikane zaidi jambo ambalo
litaongeza idadi kubwa ya wanafunzi watakaojiunga na chuo hicho.
Vile vile waajiri waliotembelea kuona shughuli
mbalimbali zinazofanywa chuoni hapo, waliushauri uongozi kufanya jitihada za
kutangaza bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanafunzi chuoni hapo ambazo baadhi
ni za viwango.
Hadi sasa chuo hicho chenye zaidi ya wanafunzi 700 kinaendesha kozi mbalimbali zinazoshirikisha wavulana na wasichana. Baadhi ya kozi hizo ni; uselemala, umeme, umeme wa jua, ufundi bomba, udereva, uchomeleaji vyuma, ushonaji nguo, electronics, ICT, fundi wa magari,food processing pamoja,upambaji pamoja na ujenzi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇