Waziri mpya wa Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi, Eng. Dk. Leonard Chamuriho,
akikabidhiwa shada la maua na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Ujenzi), Elius Mwakalinga wakati yeye na Naibu Waziri
wa wizara hiyo, Godfrey Msongwe wakikaribishwa Makao Makuu ya Wizara hiyo eneo
la Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma leo asubuhi Desemba 10, 2020. Eng.
Chamuriho alikuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Uchukuzi).Dk. Chamuriho amewataka
watumishi wa wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wafanye kazi kwa bidii na kwa weledi pia
amewataka kila mmoja kujitathmini na kwamba hatosita kwa yeyote atakayezembea
kumchukulia hatua. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA CCM BLOG DODOMA
Waziri mpya wa Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi, Eng. Dk. Leonard Chamuriho,
akikabidhiwa kadi maalumu ya ukaribisho.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey
Msongwe (kulia), akikabidhiwa shada la maua na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
(Ujenzi), Elius Mwakalinga wakati yeye na
Waziri mpya wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi,
Eng. Dk. Leonard Chamuriho,wakikaribishwa Makao Makuu ya Wizara hiyo
eneo la Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma leo asubuhi Desemba 10, 2020.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey
Msongwe (kulia), akikabidhiwa kadi maalumu ya ukaribisho.
Waziri Dk. Chamuriho na Naibu Waziri
Msongwe wakiwa katika picha za pamoja na watumishi wa wizara hiyo wa sekta ya
Uchukuzi na Ujenzi. Wizara hiyo awali ilikuwa inaitwa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano. Uapisho wa maaziri hao umefanyika jana Ikulu ya
Chamwino, Dodoma.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo anayeshugulia
Ujenzi, Eng. Mwakalinga akitoa neon la
utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu
Waziri, Msongwe na Waziri Chamuriho kuzungumza na menejimenti ya wizara hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇