LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 30, 2020

SIMBA SC YAWAZIMA WANIGERIA KWAO, YAICHABANGA PLATEAU UNITED 1-0

 


Na Mwandishi Wetu, JOS
SIMBA SC imetanguliza mguu mmoja mbele Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Plateau United jioni ya leo Uwanja wa Kimataifa wa Jos International, Jijini Jos nchini Nigeria
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mzambia Clatous Chota Chama dakija ya 53 akimalizia kazi nzuri ya winga kutoka Msumbiji, Luis Jose Miquissone.
Sasa mabingwa wa Tanzania watakuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Wakifanikiwa kuitoa Plateau United, SImba SC watakutana na mshindi kati ya Costa do Sol ya Msumbiji na Platinum FC ya Zimbabwe kuwania kuingia Hatua ya 16 Bora inayochezwa kwa mtindo wa makundi.

Mechi ya kwanza jana, Platinum FC walishinda 2-1 ugenini Uwanja wa Taifa wa Zimpeto Jijini Maputo, Msumbiji na timu hizo zitarudiana Desemba 5 Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare, Zimbabwe. 
Kikosi cha Plateau United kilikuwa; Adamu Abubakar, Ibrahim Babawo, Dennis Nya, Andrew Ikefe, Gabriel Wassa, Isah Ndala, Oche Ochewechi/Sunday Anthony, Sunday Adetunji, Abba Umar, Uche Onuasonya na Saheed Jibrin.
Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Erasto Nyoni, John Bocco, Clatous Chama nba Luis Miquissone.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages