CCM Blog, Dar es Salaam
Mpambano wa watani wa jadi Simba na Yanga umemalizika leo kwa timu hizo kutoka suluhu ya bao 1-1 katika mechi hiyo iliyopigwa leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Beki wa Kimatifa wa Kenya Joash Onyango ndiye aliyeisaidia Simba kunusurika na kichapo kutoka kwa watani zao Yanga baada ya kusawazisha bao katika dakika za lala salama na kufanya timu hizo kutoka sare hiyo ya kufungana 1-1.
Kipindi cha kwanza kilikuwa bora kwa Yanga na waliweza kupata bao kupitia kwa Mshambuliaji wao Michael Sarpong dakika ya 31 kwa mkwaju wa Penati baaada ya Tuisila Kisinda baada ya kuangushwa na Joash Onyango. Hadi timu zinaenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko huku Simba wakionekana kuliandama lango la Yanga na mnamo dakikia ya 86 Joash Onyango aliwanyanyua mashabiki wa Simba akifunga bao kwa kichwa akimalizia kona iliyopigwa na Luis Miqussone.
Mpaka dakika 90 zinamalizika watani wa jadi wameweza kugawana pointi moja moja kwa matokeo hayo Yanga wanabaki na Pointi 24 nafasi ya pili huku Simba wakifikisha pointi 20 nafasi ya tatu na Azam FC bado anaongoza Ligi kwa kuwa na Pointi 25.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇