LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 8, 2020

BIDEN ASHINDA URAIS MAREKANI, TRUMP APINGA MATOKEO


Mgombea Urais wa Chama cha Democratic nchini Marekani Joe Biden ameshinda uchaguzi wa Marekani na kuwa rais mteule wa Marekani baada ya kumshinda Donald Trump.

Joe Biden ameshinda katika jimbo muhimu la Pennsylvania, akijizolea kura zaidi ya 270 zilizohitajika ili kuchukua kiti cha White House.
Kampeni ya Donald Trump imeonesha mgombea wao hana mpango wa kukubali matokeo ya uchaguzi huo. Matokeo hayo yanamfanya Trump kuwa rais wa kwanza kutumikia awamu moja madarakani tangu miaka ya 1990.

Uchaguzi huu umeshuhudia watu wengi wakijitokeza kupiga kura tangu miaka ya 1900. 

Aidha, Joe Biden ameshinda zaidi ya kura milioni 73 mpaka sasa, idadi ya juu kuwahi kutokea kwa mgombea yoyote yule Marekani. Trump akipata kura zaidi ya milioni 70 akishika nafasi ya pili kwa idadi kubwa katika historia ya Marekani.

Rais Trump alijitangaza mshindi wa Uchaguzi wakati kura zikiendelea kuhesabiwa. Wakati wote amedai kuwa zoezi la kuhesabu kura limekuwa na dosari, lakini hajawasilisha ushahidi wowote kuhusu madai yake.

Timu ya kampeni imefungua kesi katika majimbo mbalimbali mapema Ijumaa, wakati Joe Biden alipokuwa akikaribia kunyakua ushindi huku akisisitiza uchaguzi huo haujaisha. Kwa matokeo hayo, Joe Biden anakuwa Rais wa 46 wa Marekani

Joe Biden ni nani?
Joseph Robinette Biden Jr (Joe Biden) ni mwanasiasa wa Marekani ambaye alihudumu nafasi ya 47 ya Makamu wa Rais nchini Marekani chini ya utawala wa Rais Barack Obama kuanzia 2009 Hadi 2017. Ni mwanachama hai wa Chama cha Democratic ambaye kabla alikuwa Seneta wa Jimbo la Delaware kuanzia 1973 hadi 2009.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages