LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 1, 2020

RAIS UHURU KENYATTA WA KENYA AMPONGEZA DK. MAGUFULI KWA USHINDI

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa na Rais aliyemaliza muda wake wa awamu ya kwanza, Rais Mteule Dk. John Magufuli alipofanya ziara binafsi ya siku mbili nchini Tanzania mwaka jana.

Dar es Salaam, Tanzania

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amemtumia salamu za heri kwa rais mwenzake wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kushinda uchaguzi uliofanyika Jumatano, Oktoba 28, 2020.

Rais Kenyatta amesema kuchaguliwa tena kwa Magufuli ni ishara ya upendo na imani waliyo nayo Watanzania kwa uongozi wake.

"Kwa niaba ya Watu, Serikali ya Kenya na Mimi mwenyewe nampongeza ndugu yangu, Dkt John Pombe Magufuli kwa ushindi wako na wa Chama Cha Mapinduzi, katika uchaguzi uliomalizika", alisema rais Kenyatta.

Aliongeza kuandika: ''Nchi ya Kenya inatarajia kuendelea kufanya kazi na Utawala wako kwa faida ya watu wa mataifa yetu mawili, kwa ustawi wa Afrika Mashariki na kwa amani, utulivu na ukuaji wa bara la Afrika.

Rais Kenyatta pia amemtakia rais mwenzake wa Tanzania afya njema na ufanisi anapojiandaa kuhudumu kwa muhula wa pili madarakani na kumhakikishia ushirikiano wa Kenya na kwa utawala wake .

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages