Rais Dk. John Magufuli (Pichani), kesho, Ijumaa, Novemba 13, 2020, atalizindua rasmi Bunge la 12 la jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kulihutubia Taifa kupitia Bunge hilo, Bungeni jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewaambia wabunge katika kikao cha tatu, kilichofanyika leo, kwamba Rais Dk. Magufuli ataanza saa 4:00 kutoa Hotuba yake na kuwataka Wabunge kuhakikisha kila mmoja ameingia Bungeni Saa 3 asubuhi ili kuwa tayari kwa hotuba hiyo.
"Waheshimiwa Wabunge, sasa naahirisha kikao hiki cha Bunge ili kupisha maandalizi ya ukumbi huu kwa ajili ugeni huu wa Mheshimiwa Rais, na ninawaombeni kesho mjitahidi kuwahi kufika Bungeni saa 3:00 asubuhi kwa sababu shughuli hiyo ya kesho ni muhimu sana", alisema Ndugai.
Mapema Bungeni leo, Spika wa Bunge alipokea barua kutoka kwa rais Dk. John Magufuli ya pendekezo la jina la Waziri Mkuu wa Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo baada ya kuifungua alimtangaza Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa ndiye aliyependekezwa na Rais Dk. Magufuli.
Kufuatia pendekezo hilo la Rais Dk, Magufuli, Bunge lilifanya uchaguzi uliompitisha Majaliwa kwa kura 354 zilizopigwa na wajumbe wa Bunge (MB) na kumfanya Majaliwa kuwa amepita kwa asilimia 100.
Baadaye ulifanyika Uchaguzi wa Naibu Spika ambapo Dk. Tulia akson aliyekuwa mgombea pekee, naye alipigiwa kura na Wajumbe wa Bunge (MB) na kumchagua kwa kura 350, akiwa amekosa kura nne tu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇