LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 15, 2020

NMB NDANI YA DODOMA

Benki ya NMB jana imeandaa hafla maalum jijini Dodoma ya kuwakaribisha Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la 12, lililozinduliwa hivi karibu na Rais John Pombe Magufuli, kwa ajili ya kuwapongeza kwa kuchaguliwa kuwawakilisha wananchi na kuwatakia safari njema katika kipindi cha miaka mitano ijayo. 


Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson akikaribishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna.  Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB Dk. Edwin Mhede.


 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akimkaribisha Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania - Dk. Benard Kibesse. Wakishuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB Dk. Edwin Mhede(kulia), Afisa  Mkuu wa Wateja Binafsi  na Biashara wa NMB - Filbert Mponzi(kushoto) na Mkuu wa Idara wa Mawasiliano wa NMB - Eunice Chiume.

 

Hafla hiyo, ilizinduliwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Tulia Ackson aliyekuwa Mgeni rasmi. Benki ya NMB ilitumia fursa hiyo kuwajulisha Waheshimiwa Wabunge namna wanaweza kufaidika  na huduma nyingi za NMB ikwemo; mikopo maalum, uwekezaji, bima mbalimbali, na matumizi mbadala ya kibenki  kama NMB Mkononi.




Waheshimiwa Wabunge wakiburudika katika hafla hiyo


Akizungumza kwa niaba ya Benki ya NMB, Afisa Mkuu Mtendaji, Bi. Ruth Zaipuna alisema, moja ya malengo ya Benki hiyo ni kuhakikisha wanashirikiana na  wadau katika kujenga taifa bora lenye uchumi imara kupitia sekta ya kibenki. Dhamira ya NMB ni kuendelea kushiriki katika miradi ya maendeleo katika majimbo yao na taifa kwa ujumla.

 

Vile vile, Dk. Tulia aliipoongeza Benki hiyo kwa kuendelea kuboresha huduma zake na kujitanua kiutendaji katika kila eneo hapa nchini huku akitambua mchango wa NMB katika jamii. 





Wakiwa Dodoma, Zaipuna na Mponzi walishuhudia uzinduzi wa Bunge la 12, na vile vile kupata nafasi ya kumtembelea Kamishna Generali wa Magereza nchini – Suleimani Mzee katika ofisi yake.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages