LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 15, 2020

KONGAMANO LA WHA LA KUWANOA KINAMAMA WA VIKUNDI VYA VIKOBA NA UJASIRIAMALI LILIVYONOGA, DAR, MBELE YA DC GODWE



Mwenyekiti wa Chama cha Women of Hope Alive (WHA) Mbunge wa Viti maalum (CCM), Janeth Mahawanga (kulia), akimkaribisha Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule baada ya kuwasili kwenye Kongamano la kuwanoa wanawake wa Vikundi vya Vikoba na Ujasriamali, lilofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, jana.
Mbunge wa Viti Maalum ( CCM), Janeth Mahawanga (kulia), akijadiliana jambo na Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Grace Haule baada ya Katibu huyo kuwasili kwenye Kongamano la kuwanoa wanawake wa Vikundi vya Vikoba na Ujasriamali, lilofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Ndugu Ngoda, Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akisalimiana na na Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Grace Haule baada ya kuwasili na kutoa udhuru wa mkuu wa mkoa huyo kutoweza kufika katika Kongamano hilo, lakini kutokana na umuhimu wa shughuli hiyo ambaye alimwakilisha vilivyo. Kulia ni Mwenyekiti wa WHA, Mbunge wa Viti Maalum Janeth Mahawanga akifurahia ugeni huo.
"Mkuu wa mkoa  Bwana Abubakari Kunenge, hataweza kuja, lakini ametuma Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bwana Godwin Gondwe kuja kumwakilisha, bila shaka mambo yatakwenda vizuri", akasema mwakilishi huyo wa mkuu wa mkoa kumwambia Mbunge Janeth Mahawanga kwa tabasam.
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam akiandaa mabo fulani fulani katika Kongamano hilo.

 ☝Mwenyekiti wa WHA, Mbunge wa Viti Maalum Janeth Mahawanga akifungua rasmi Kongamano hilo. Nyuma yake ni wana kamati ya maandalizi ya Kongamano hilo.👇

 
Mwenyekiti wa WHA, Mbunge wa Viti Maalum Janeth Mahawanga akisindikizwa kwa shangwe na Wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo baada ya kulifungua rasmi👇

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo Farida Akida ambaye pia alikuwa MC wa Kongamano hilo akiendelea kunogesha shughuli.
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace akiwa na baadhi ya wadau katika Kongamano hilo.

Wadau mbalimbali wakijisajili wakati wa kuingia ukumbini kwenye Kongamano hilo👇


Watoa mada mbalimbali wakiwa tayari ukumbini kwenye Kongamano hilo👇
Watoa mada hao, kutoka kushoto ni Mwana Saikolojia Sadaka Gandi, Dk. Marina Njelekela kutoka  Chama Cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) na mwakiliishi kutoka Jubilee Life  Insurance

Dk. Marina Njelekela (kushoto), kutoka  Chama Cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) akitoa mada kwa kushirikiana na Msaikolojia Sadaka Gandi (kushoto) kuhusu afya ya akili na umuhimu wa afya hiyo kuwa vizuri ili mwanamke aweze kufanikisha vema masuala ya Vikoba na Ujasiriamali.

Picha mbalimbali za Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo wakiwapongeza Dk. Njelekela na Gandi baada ya kumaliza kutoa mada.👇


Kisha inaingia zamu ya Mtaalam kutoka Jubilee Insurance naye kutoa mada kuhusu masuala ya Bima hasa katika masuala ya Biashara na Ujasiriamali👇

Mtaalam huyo kutoka Jubilee Life Insurance akiteta kidogo na Mwemnyekiti wa WHA, Mbunge janeth Mahawanga kabla ya kwenda kutoa mada yake kwa kina mama kwenye Kongamano hilo. Kisha akaendelea na utoaji mada👇



Mtaalam wa vikundi na masuala ya usajili wa vikundivya Ujasiriamali na Vikoba, Evans Chipindi akitoa mada kwenye Kongamano hilo👇


Picha mbali mbali Wanavikundi vya Vikoba na Ujasiriamali kutoka Dar es Salaam, Pwani na Morogoro, Waalikwa na Wataalam mbalimbali wakiwa wametulia ukumbini katika Kongamano hilo.👇













Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Godwe akiwasili ukumbini kunogesha Kongamano hilo👇
Mwenyekiti wa WHA Mbunge Janeth Mahawanga na Katibu wa Jumuiya ya  CCM ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule wakimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe baada ya kuwasili kwenye Kongamano hilo.

DC Gondwe akisalimia wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo baada ya nkuwasili. Kushoto ni Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule

DC Gondwe akisalimia baada ya kuwasili ukumbini huku akisindikizwa na Mwenyekiti wa WHA Mbunge Janeth Mahawanga na katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule (kulia). Janeth pia ni Mwenyekiti wa UWT Kata ya makongo.

DC Gondwe akisalimia baada ya kuwasili ukumbini huku akisindikizwa na Mwenyekiti wa WHA Mbunge Janeth Mahawanga na katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule (kulia). Janeth pia ni Mwenyekiti wa UWT Kata ya Makongo jijini Dar es Salaam.

Meza Kuu👇

DC Gondwe akiwa amesimama meza Kuu pamoja na wenyeji wake Mwenyekiti wa WHA Mbunge Janeth Mahawanga (kuhsoto) na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule huku wakishangilia baada ya kufika meza kuu kwenye Kongamano hilo. Janeth pia ni Mwenyekiti wa UWT Kata ya Makongo jijini Dar es Salaam.

DC Gondwe akiwa amekaa meza Kuu pamoja na wenyeji wake Mwenyekiti wa WHA Mbunge Janeth Mahawanga (kuhsoto) na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule, baada ya kufika meza kuu kwenye Kongamano hilo. . Janeth pia ni Mwenyekiti wa UWT Kata ya Makongo jijini Dar es Salaam.

DC Gondwe akishauriana jambo na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa WHA Mbunge Janeth Mahawanga ili kuweka sawa baadhi ya mambo baada ya kuwasili kwenye Kongamano hilo. Kulia ni Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule. Janeth pia ni Mwenyekiti wa UWT Kata ya Makongo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa WHA Mbunge Janeth Mahawanga akizungumza kumkaribisha DC Gondwe kuzungumza na Wana Kongamano. Janeth pia ni Mwenyekiti wa UWT Kata ya Makongo jijini Dar es Salaam.

DC Gondwe akiselebuka kidogo sanjari na muziki uliokuwa ukitumbuiwa kumsindikiza kwenda kuzungumza  na wanakongamano hilo huku akisindikizwa jukwaani na Mwenyekiti wa WHA Mbunge Janeth Mahawanga (kuhsoto) na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule (wapili kulia).

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo Farida Akida ambaye pia alikuwa MC wa Kongamano hilo,akikabidhi 'mike' kwa Mbunge Janeth Mahawanga ili amkabidhi DC Gondwe.

Mwenyekiti wa WHA Mbunge Janeth Mahawanga (kuhsoto) akikabidhi 'mike' kwa DC Gondwe ili azungumze na wana Kongamano hilo. Kulia ni  Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule.

DC Gondwe ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, abubakar Kunenge akizungumza na Wana Kongamano hilo.

 Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule akizungumza  kutoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi DC Gondwe, huku DC huyo akimtazama kwa makini wakati wa Kongamano hilo. Kushoto ni Mwenyekiti wa WHA Mbunge Janeth Mahawanga. 

DC Gondwe na viongozi wenzake katika meza kuu wakirahia maneno ya shukurani aliyokuwa akitoa Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Geace Haule

Kisha Wana Kongamano wakilipuka kumpongeza Grace bila shaka kwa maneno yake murua ya shukrani aliyoyatoa kwa mgeni rasmi👇


Burudani ya muziki ulioporomoshwa na Bendi ya Muziki wa dansi ya Kimondo Sound kuwapunguzia uchovu wanakongamano hilo.👇















Watoa huduma za aina mbalimblai wakiwa kazini kwenye Kongamano hilo.👇
Rehema nalaila Kiula (Kushoto) na Rahini Chudasama (kulia) wakihudumia wateja kwenye eneo lao la maonyesho ya bidhaa za afya na urembo kwenye Kongamano hilo.

Watumishi wa Diamond Jubilee Life Insurancewakiwajibika katika eneo lao la maonyesho katika Kongamano hilo.





Meneja Mauzo wa BancABC Bertha Bash akiwa na watumishi wenzake kwenye banda la benki hoyo kwenye Kongamano hilo.

Mtaalam wa Sara Nassor wa kampuni inayoshughulika na tiba za Kisunna, akimuonyesha mteja kifaa cha kuondoa damu chafu mwilini kinavyotumika, mdau huyo Jimmy Henry  alipotembelea banda lililokuwa linatoa huduma hiyo katika Kongamano hilo. Anayeshuhudia ni Naomi Amash wa Weruweru Hotel mkoani Kilimanjaro.👇

MC Farida Akida akiwatambulisha Kamati ya Maadalizi ya Lonhgamano hilo.👇





Msosi kwa Wote mwishoni mwa kongamano hilo Wakitanguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe👇





Diwani wa Ilala Beatrice Edward akipata chakula kilichoandaliwa akwa wanakongamano. katika Kongamano hilo Walialikwa pia madiwani wapya kwa ajili ya kupata maarifa na mbinu mbalimbali za kusaidia wajasiariamali katika maeneo yao.


Mishoni mwa Kongamano👇
DC Gondwe akimshukuru Mwenyekiti wa WHA, Mbunge Janeth Mahawanga akiwa tayari kuondoka baada ya kuamliza kazi yake. Kulia ni Katibu wa UWT mkoa wa Dare Salaam Grace Haule.
 

Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo wakimsindikiza DC Gondwe wakati akiondoka ukumbini.

Picha za kumbukumbu DC wa Temeke GOdwin Gondwe , Mbunge Janeth Mahawanga na Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo👇



MWISHO...

Ziada: Msimamizi Mkuu wa Blog hii ya Taifa ya CCM (CCM Blog) Bashir Nkoromo, kwa niaba ya timu yote ya CCM Blog anampongeza Mheshimiwa Mbunge Janeth Mahawanaga kwa kuandaa kongamano hilo ambalo linasaidia sana katika kuwakomboa Wanawake na Taifa kwa ujumla kiuchumi. Kwa Manoni au hitaji lolote kuhusu chapisho hili au chochote, Tupigie 0712 498008 au 0789 498008, Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages